Wananchi wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wameaswa kuachana na tabia ya ukataji wa mitiovyo badala yake wawe mstari wa mbele wa kuwa na utamaduni wa upandaji wa miche mbalimbali ya miti ili kurudisha uoto wa asili uliopotea sambamba na utunzaji wa mazingira ili kuufanya mkoa wa Mtwara uwe na muonekano wa kijani.
Wito huo ulitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Gelasius Byakanwa alipokuwa akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Muungano kilichopo Kata yaLulindi halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwenye sherehe za maadhimisho ya uzinduzi wa upandaji miti kimkoa ambapo Mkuu wa Mkoa huyo ndio aliongoza zoezi la upandaji miti akiambatana na viongozi mbalimbali za wilaya zote za Mkoa waMtwara na kushiriki kwa vitendo katika kupanda miche hiyo ya miti zaidi ya 200.
Alisema kuwa kutokana na hali ya mazingira kuendelea kuwa mbaya hasa kwa ukosefu wa miti kwenye maeneo mbalimbali mkoani Mtwara kutokana na tabia ya ukutajimiti ovyo jambo ambalo limepelekea uwepo wa athari za mazingira kwa sasa, kunahaja ya kuweka mkakati madhubuti utakaosaidia kutunza mazingira kuwa borazaidi.
Mhe. Byakanwa alisema kila wilaya ndani ya mkoa wa Mtwara inatakiwa kuweka mkakati wa upandaji miti katika maeneo mbalimbali ikiwemo maeneo ya shule za Msingi na Sekondari pamoja na sehemu zingine ambazo zitafaa kwa ajili ya upandaji wamiche ya miti hali hiyo itasiaida na kufanya sehemu kubwa ya mkoa wa Mtwara kuwa katika hali ya kupendeza ya ukijani.
Alisema mkoa umejiwekea mkakati wa upandaji wa miti kila mwaka iwe imeshapanda miche ya miti ifikayo zaidi ya miche milioni 6.5 hivyo halmashauri za wilaya, miji na manispaa zilizopo katika mkoa wa Mtwara zenyewe zitapaswa kuwana mkakati wa upandaji wa miche ya miti milioni 1.5 kila moja kwa mwaka.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kupitia mkakati huo utasaidia kurejesha hali ya miti iiyopotea kwenye mkoa wa Mtwara unaosababishwa na baadhi ya wananchi kuwa na tabia ya kukata miti ovyo kwa ajili ya matumizi ya kuchoma mkaa na ukataji wakuni ili kufanya biashara.
“Mkakati huu tukianza nao utatufanya baada ya miaka kadhaa mkoa wa Mtwara utakuwa umerejea na kuwa na miti mingi katika maeneo mbalimbali lakini pia nataka wananchi kulinda mazingira hasa vyanzo vya maji na kuacha tabia yakukata miti ovyo,”alisema Byakanwa
Aidha, Mhe.Byakanwa alisema ili kuweza kuwa na utaratibu mzuri wa kudhibiti athari za ukataji miti ovyo inabidi tuwe na mpango unaoanzia ngazi ya kijiji kwa kuanza kuwa na kamati za kudhibiti misitu za vijiji ambazo zitaweka utaratibu wa ukataji miti pale mtu atakapohitaji hata kama miti hiyo ipo kwenye shamba lake mwenyewe.
Alisema Wakuu wa Wilaya kwa kushirikiana na Wakurugenzi na watendaji wengine ndani ya kila Wilaya na Halmashauri wawe mstari mbele katika kuhamasisha jamii na wananchi kwa ujumla kutunza miti na kupanda miche ya miti ili kuweka mazingira yawe bora.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa