Mkuuwa mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa amewahakikishia wananchi wa kata yaNangoo wilayani Masasi kuwa watalipwa fidia ya maeneo na Mali zilizoharibiwawakati wa utekelezaji wa mradi wa maji wa Mbwinji unaotumiwa na wananchi waMasasi na Nachingwea.
MKuuwa mkoa ametoa kauli hiyo baaada ya kupokea malalamiko kutoka kwa wananchi wakata hiyo yaliyoainishwa katika makundi matatu ikiwemo watu kulipwa pungufu,kulipwa wasiostahili na wengine kutolipwa kabisa wakati ni wahanga.
Kufuatiahali hiyo Byakanwa amewaeleza wananchi wa kata hiyo na Kata jirani kuwaatahakikisha kila mtu anayestahili kulipwa analipwa ndani ya miezi miwili baadaya uchunguzi wa kutambua waliolipwa wakati hawana sifa kukamilika ambapo ndaniya miezi hiyo miwili watakuwa wamebainika na hatua zitachukuliwa.
MheByakanwa amesema "Nipeni hii miezi miwili nikipata kibali kutoka kwaMkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU tutashughulikia ngazi ya Mkoa kwa kuunda kamatiitakayo fanya uchunguzi na kutambua wale wanaostahili na wasiostahili na hatuazitachukuliwa hapahapa bila kusubiri utaratibu wa TAKUKURU ambazo zina chukuaunamlolongo mrefu"
Wananchiwametoa malalamiko kuwa kuna watu ambao hawakupitiwa na mradi walilipwa fedhawakati wanaostahili hawajalipwa litafanyiwa kazi haraka na watarudisha fedhahizo ili walipwe wanaostahili.
AKijibuhoja ya kulipa fidia watu hewa Mwakilishi wa ofisi ya TAKUKURU Masasi ameelezakuwa uchunguzi unaendelea wa kuwabaini watu hao na kwa kijiji cha Liputukilichopo Kata ya ndanda wilayani humo umekamilka na imebainika kweli kuwa wapowatu ambao walilipwa bila kuwa na maeneo yaliyoathiriwa na mradi.
Aidhamhe. Byakanwa amemwagiza Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha anafungua vioskivya maji vyote vilivyofungwa kwasababu ya wauza maji wamekila hela ili wananchiwaendee kupata huduma ya maji kama serikali ya awamu ya tano inavyoelekeza kuwawananchi lazima wapate maji kwani wanaadhibiwa kwa kosa ambalo hawajatenda.
PiaMhe. Byananwa amemsisitiza Mkurugenzi wa MANAWASA kuhakikisha wale wauza majiwote waliokula fedha wakamatwe ili walejeshe fedha hizo haraka na baada ya wikimbili zoezi hilo liwe limekamilika.
Mhe.Byakanwa amewataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na miundombinu ya majikwani jamii ndio yenye jukumu la kutunza kwa kuto fanya shughuli zozote karibuna vyanzo vya Maji lakini pia kuilinda miundombinu yake kwani serikali inatumiafedha nyingi kutekeleza Miradi hiyo.
Mradiwa Mbwiji ulianza kutekelezwa 2011 mwaka na ulighalimu zaidi ya bilioni 30.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa