Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) imetoa mafunzo ya Matumizi ya Mfumo mpya wa Kielektoniki wa Manunuzi ya Umma (NeST) kwa Watumishi wapatao 700 kutoka vituo vya kutolea huduma ngazi ya msingi, wazabuni pamoja na mafundi ujenzi wa Majengo.
Mafunzo hayo ambayo yametolewa kwa muda wa siku tatu (3) kuanzia tarehe 10 - 12 march 2025 yamefanyikia katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo uliopo masasi mjini.
Awali akizungumza katika siku ya kwanza ya ufunguzi wa mafunzo hayo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Rashid Njozi amesema anawashukuru PPRA kwa kutoa mafunzo hayo ya mfumo wa NeST katika Halmashauri hiyo ambao utarahisisha Manunuzi ya Umma .
"Leo nimefungua mafunzo yanayohusiana na NeST, mafunzo haya yanaendeshwa na PPRA na yanatolewa kwa Walimu wakuu, wakuu wa shule, Watendaji wa Vijiji na kata, na mwisho kwa wazabuni pamoja na mafundi ujenzi wa Majengo na hapa nimesisitiza watumie fursa hii vizuri kwa maana mfumo huu utarahisisha kazi yakuweza kufanya manunuzi yote yanayohusu vifaa vya Serikali na huduma zingine mbalimbali tutazitangaza".
Naye Bw.Fenias Manasseh ambaye ndiye Meneja wa PPRA kanda ya kusini amesema, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma inawajibu wa kuhakikisha Taasisi nunuzi wanatekeleza majukumu yao katika Ununuzi wa Umma kwa kuzingatia Sheria na taratibu.
"Tumekuja hapa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vituo vya kutolea huduma lengo ni kuwapitisha kwenye mfumo wa NeST ili waujue unavyofanya kazi na hatmaye waweze kutekeleza miradi ambayo ipo kwa ajili ya kuleta maslahi kwa Wananchi kwa kufuata kanuni na taratibu zote za Ununuzi wa Umma "
Amesema kwa upande wa Wazabuni na mafundi ujenzi wa Majengo (Lacal fundi) nao wamepatiwa mafunzo hayo na kuwaambia fursa zilizopo Serikalini kupitia sheria kwenye mfumo wa NeST.
12/03/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa