Licha ya sheria ya manunuzi na.10 ya mwaka 2023 iliyosainiwa na kuanza kutumika Oktoba 06, 2023 ambayo inataka matumizi ya mfumo mpya wa manunuzi ya kielektroniki (NeST) ndio utumike hasa kwenye taasisi za umma kwenye mambo yote ya uzabuni na ununuzi kwa kuachana na matumizi ya karatasi imeelezwa kwamba zipo baadhi ya taratibu zinashindwa kufanyika ndani yake kutokana na
kutoufahamu na mkwamo mkubwa zaidi upo kwenye mtiririko wa uzabuni.
Kufuatia changamoto hizo Ofisi ya Rais- TAMISEMI kwa kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa manunuzi ya umma (PPRA) imefanya ziara ya kutembelea na kukutana na Wataalamu wa ngazi ya Halmashauri na watumiaji wa mfumo katika ngazi za vituo vya kutolea huduma na lengo kubwa likiwa ni kujadiliana, kushauriana na kuweka mpango wa kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika matumizi ya mfumo.
Katika picha ni baadhi ya Wataalamu, na watumiaji wa mfumo kutoka ngazi ya Halmashauri ya Wilaya Masasi, Halmashauri ya mji Masasi, na Nanyumbu wamekutanishwa hapo kwa pamoja Jana tarehe 18/12/2024 katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya wasichana Masasi mjini wakipatiwa mafunzo namna ya uendeshaji mfumo, kutafsiri sheria ya manunuzi na kutekeleza kwa kuzingatia mfumo wa NeST, jinsi ya kutathimini mikataba ya ununuzi na namna ya kuitekeleza kwa kufuata misingi na taratibu zote za kizabuni.
Bw.Hamis Ally kutoka TAMISEMI ndiye mwezeshaji wa mafunzo hayo amesema mfumo huo unalenga kuongeza ufanisi katika sekta ya manunuzi, kudhibiti rushwa na kurahisisha Mchakato wa uzabuni kwa uwazi lakini umeonekana kuwa changamoto kwa maofisa manunuzi kwenye taasisi mbalimbali za umma na binafsi na ndio maana tupo tunatoa mafunzo haya ili kuzisaidia taasisi zifikie malengo waliyojiwekea.
Aidha sekta ya manunuzi ambayo inachukua zaidi ya asilimia kubwa ya bajeti katika taasisi
na ili kuhakikisha inasaidia kutimiza malengo yake kwa kufuata misingi ya manunuzi Kila taasisi zimekumbushwa kutenga bajeti za kusaidia mafunzo Kama hayo kwa Watumishi wao ili taasisi ziweze kufikia dira na matarajio Yao.
Hata hivyo katika mafunzo hayo washiriki pia wamepata nafasi ya kuorodhesha changamoto zote ambazo wanakutana nazo katika mfumo ili Serikali iendelee kuzitafutia ufumbuzi.
Ifahamike kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI imekuwa ikitekeleza miradi ya ujenzi wa miundo mbinu ya Shule za Msingi, Shule za Sekondari pamoja na vituo vya kutolea huduma za Afya kwa kutumia rasilimali za ndani (Force account) ambapo vituo hivyo vimeelekezwa kutumia mfumo wa NeST Mobile App kwenye ununuzi wa bidhaa na huduma katika miradi na Shughuli Nyingine za Kituo.
Kutoka: Kitengo Cha Habari, Mawasiliano (W) Masasi
19/12/2024.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa