Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Mhe.Ibrahimu Chiputula amesema Katika kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Nov 27,2024 Halmashauri ya Wilaya Masasi ina matarajio makubwa kuona uchaguzi huo unafanyika kwa amani na utulivu mkubwa.
Chiputula ametoa kauli hiyo mapema leo hii Sept 26, 2024 katika kikao kilichoongozwa na msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri hiyo Bi.Beatrice Mwinuka wakati akitoa maelekezo muhimu kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa uwazi, haki na usawa kwa kuzingatia sheria na taratibu za Uchaguzi zilizowekwa.
Amesema "Sisi tulio hapa ni watu wachache sana miongoni mwa wengi walioko huko nje, lakini tumepata heshima kubwa yakuitwa hapa, naomba mkaitendee haki hiyo heshima mliyopewa, yameitwa makundi mbalimbali kwa dhamira ujumbe ukafike kwenye maeneo husika na matarajio yetu kuona kwenye Halmashauri yetu uchaguzi huo wa Serikali za Mitaa unakwenda kwa amani na utulivu ndio kwasababu dhamira yetu, usiwe sehemu yakutengeneza chuki baina yetu na ndio maana hapa leo tupo makundi mchanganyiko naomba tukawe wakweli kwenye hayo mambo na tufanye kwa mujibu wa taratibu na kanuni"....amesema Chiputula
Ameongeza kuwa viongozi wa Vyama vya Siasa wanapaswa kutambua kuwa wameitwa kushiriki katika kikao hicho kutokana na nafasi zao kwenye Jamii, na uchaguzi huo unakwenda kushindanisha vyama na watu watakaochaguliwa wanatokana na Chama hivyo wafahamu dhamira kuu ni kumtafuta kiongozi na yeyote atakayepatikana atakuwa ni mtanzania hivyo hakuna sababu ya Kuleta malumbano ili Halmashauri ya Wilaya Masasi iendelee kung'aa na kuonekana kwenye uso wa dunia kwamba wametekeleza jukumu hilo kwa amani na utulivu.
Hata hivyo mhe Chiputula amehitimisha kwa kuendelea kuwaomba viongozi walioshiriki kikao hicho wakiwemo mamwenye, wazeee maarufu, viongozi wa dini, Watendaji wakasaidie Kutoa mwongozo kwa Jamii juu ya zoezi la uchaguzi wa Serikali za Mitaa Lakini pia wanayo nafasi ya kuzuia vijana wanaoanzisha vurugu na fujo kwenye maeneo ya uchaguzi.
26/09/2024
@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa