KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022 Ndugu Sahil Nyanzabara Geraruma amekagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri ambapo Mwenge wa mwaka huu 2022 umeambatana na kauli mbiu inayosema “Sensa ni Msingi wa mipango ya maendeleo shiriki kuhesabiwa tuyafikie malengo ya Taifa”. Mwenge ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya Masasi umekimbizwa umbali wa kilomita 118.5 kwa kupita katika vijiji 13, kata 10 na tarafa 3. Aidha Mwenge wa Uhuru Kitaifa umepita katika miradi minne (4) ambapo kati ya hiyo, mradi mmoja (1) utawekewa jiwe la msingi, mradi mmoja (1) utakaguliwa na kuonwa, na miradi miwili (2) itazinduliwa. Gharama za miradi iliyopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru ina thamani Tshs. 482,100,000/= Serikali Kuu Tshs. 290,000,000 sawa na asilimia 69.59 Halmashaur Tshs. 5,000,000 sawa na asilimia 0.79 Wananchi Tshs.187,100,000 sawa asilimia 29.61
Miradi hiyo 4 iliyoandaliwa ambayo imepitiwa na Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi, imegawanyika kisekta kama ifuatavyo;Sekta ya Afya mradi1,Sekta ya Elimu mradi 1,Sekta Binafsi mradi1,Shughuli za vijana mradi 1 Aidha katika miradi hiyo 4, Msafara wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2022 umefanya kazi kama ifuatavyo; Kuweka jiwe la msingi mradi 1 Kuzindua miradi 2 Kuona, kukagua na kupata taarifa mradi 1 Jumla miradi-4
JENGO LA WAGONJWA WA NJE (OPD)
JENGO LA MAABARA
Tarehe 21.10.2021 shule ya Sekondari Chiungutwa ilipokea jumla ya Tshs 40,000,000/= kutoka Serikali Kuu (Mradi Na 5441 TCRP) kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa ,Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya Sekondari Chiungutwa ulianza rasmi mwezi Oktoba Mwaka 2021, na kukamilika Mwezi Januari 2022. Aidha Majengo haya yamejengwa kwa kutumia utaratibu wa (Force account) ambao ni mafundi wa kawaida (local fundi) wametumika na vifaa kununuliwa moja kwa moja kutoka viwandani na maduka ya jumla. Gharama kuu za Mradi ni shilingi 40,000,000/= Mradi umekuwa shirikishi mbali na ushiriki wa Kamati zilizopo kwenye mwongozo, Pia Jamii imeshiriki katika kuchimba msingi ambayo thamani yake ni Tshs100,000 .Mradi umegharimu kiasi cha fedha za Kitanzania Shilingi 38,628,828.92 na pesa iliyobakia ni kiasi cha shilingi 1,376,171.08 .
Hii ni kilabu ya wanafunzi wapinga rushwa ambapo mkimbiza mwenge wa uhuru 2022 NduguSAHILI NYANZABARA GERARUMA alipata pia fursa ya kuitembelea na kujua namna inavyojiendesha katika shule ya sekondari ya chiungutwa
Kikundi cha vijana cha Tuinuane kilianza rasmi tarehe 10/08/2019 kikiwa na wanachama watano (4 Ke na 1 Me). Shughuli kuu za kikundi zikiwa ni Utengenezaji wa batiki na kusuka makapu ,Kupitia mradi wa utengenezaji wa Batiki pamoja na Makapu kikundi kilifanikiwa kukusanya shilingi 1,100,000 kama faida ya mradi huo ndipo mnamo mwezi Novemba 2020 kikundi kilinunua Ng’ombe mmoja wa Maziwa aliyezaa aina ya Frisian hivyo kikundi kinaendelea kukamua maziwa na kuyauza kwa jamii kiasi cha Lita 10 kwa Siku.
Kituo cha mafuta Engen kipo katika kijiji cha Nagaga kata ya Namalenga Mradi huu umejengwa na kukamilika kwa gharama ya Tshs. 185,000,000/= na umefuata sheria zote za usajili wa kituo na malipo yote ya Serikali yamefanyika kikamilifu na kupewa ruhusa ya kuendesha mradi huu katika kijiji cha Nagaga ,mafanikio yanayotokana na kufungua mradi huu katika kijiji cha Nagaga.Kupunguza tatizo la uhaba wa upatikanaji wa mafuta katika kijiji cha Nagaga na vijiji jirani,Kutoa ajira za muda mrefu na muda mfupi,Mradi huu umeongeza mapato kwa serikali kwa kulipa kodi mablimbali kulingana na uhitaji.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa