WANANCHI/ WAKULIMA WOTE MKOANI MTWARA TUMIENI VIZURI FEDHA MLIZOPATA KWENYE MAUZO YA KOROSHO KWA KUJIANDAA KUTOA HUDUMA KWA WATOTO WENU WATAKAOJIUNGA NA MASOMO KUANZIA JAN 13/2025: RC SAWALA
Wananchi/ Wakulima wote Mkoani Mtwara wametakiwa kutumia vizuri fedha ambazo wamezipata kwenye mavuno ya korosho huku wakijiandaa na Kutoa huduma kwa Watoto wao watakaojiunga na masomo kuanzia shule za awali, Msingi, na Sekondari ifikapo jan 13/2025
Pia wamekumbushwa kuwa na nidhamu ya matumizi mazuri ya fedha hizo walizopata kwa kujiandaa na msimu unaofuata wa Kilimo ili kuongeza uzalishaji.
Hayo yamejiri Leo tarehe 30/12/2024 katika hafla ya uzinduzi wa msimu wa Kilimo kwa mwaka 2024/2025 Kwa Mkoa wa Mtwara, ambao uzinduzi huo umefanyika katika Kijiji Cha Mpindimbi Kata ya Mpindimbi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi huku Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu mhe.Christopher Magala ndiye mgeni rasmi akimwakilisha mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenani Sawala.
Amesema hawatapendezwa kuona Wakulima/ Wananchi ambao wamepata fedha nyingi katika msimu unaoishia kwenye mauzo ya korosho na akashindwa kumuhudumia mtoto wake kwenda shule .
"Kuna wakati mwingine mnajisahau sana, toeni kipaumbele kwenye mambo ya Elimu kwa Watoto wenu, Wakulima walio wengi kwasasa wamepata fedha nyingi Sana, tutashangaa kuona pia mtoto wa mkulima aliyepata fedha nyingi anatembea umbali mrefu Kwa miguu kama km.10- 25 kwenda shuleni kufuata Shule ilipo, sisi sote ni mashahidi shule zetu zimejengwa kwenye kila kata tena kuna baadhi ya kata ina shule zaidi ya moja na kata nyingine zina Shule moja na Watoto wengi hutembea umbali mrefu kwenda shuleni kutafuta Elimu, tumieni fedha hizi mlizopata kununua baiskeli ili Watoto waweze kuhudhuria masomo Yao" alisisitiza Mhe.Magala....
Ameongeza kuwa mafanikio hayo sasa Kwa Wakulima yametokana na Sera nzuri ya Serikali ya awamu ya sita chini ya Uongozi shupavu wa Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa kuweka mazingira mazuri katika maeneo yanayoruhusu uwekezaji kwenye Kilimo na masoko ya mazao.
" Katika msimu 2023/2024 Serikali kupitia TARI NALIENDELE ilitoa mbegu za ufuta tani 10 ambazo zilisambazwa kwenye Halmashauri zote na Wakulima walipokea pembejeo za korosho, pembejeo za ruzuku, aina ya salfa ya unga tani 21,382 na viutilifu vya Maji.
Aidha ameendelea kuelezea kuwa mifumo ya masoko ya mazao imeboreshwa Kwa kutumia minada ya wazi kwa njia ya mtandao ambayo imesaidia kuimarisha bei za ushindani na ndio maana tumeshuhudia bei imekuwa nzuri .
"Vile vile bandari yetu ya Mtwara imeendelea kusafirisha korosho zinazozalishwa kwenye mkoa wetu wa Mtwara na mikoa ya jirani, (Lindi, Mtwara na Ruvuma) kwenda kwenye masoko ya nje na kuongeza ajira na mapato ndani ya Mkoa wetu wa Mtwara ".
"Ndugu Wananchi katika kuondoa changamoto ya upatikanaji wa mbolea za mazao mchanganyiko, Serikali ya awamu ya sita imeandaa mpango wa ruzuku kwa Wakulima kwa msimu wa mwaka 2023/2024 ambapo jumla ya Wakulima 11,605 wamenufaika kwa kununua jumla ya tani 4513 na mbolea yenye thamani ya sh.bilioni 7.9 ambapo Wakulima wao walichangia sh. Bilioni 5.9 ambapo pia kwa mwaka huu 2024/2025 Serikali inaendelea tena na mfumo huu ambapo pembejeo zitatolewa kama msimu uliopita, hivyo nichukue fursa hii kuhamasisha Wakulima wote kuendelea kujisajili Kwa maafisa Kilimo ili isaidie na hatmaye kuongeza uzalishaji wa mazao."
Mwisho mhe.Magala akahitimisha Kwa Kutoa rai kwa mawakala/ wazabuni ambao wamepewa kazi ya kusambaza na kuuza pembejeo za ruzuku kuhakikisha wanafika Kila eneo walilopangiwa kwasababu Kuna tabia imejengeka kwa baadhi ya mawakala kuchagua baadhi ya Maeneo, hivyo " nitoe tahadhari hakikisheni mnatoa huduma katika Kila wilaya uliyopangiwa .
Hata hivyo uzinduzi wa msimu wa Kilimo mwaka 2024/2025 Kwa Mkoa wa Mtwara umeenda sambamba na kuzindua mafunzo kwa njia ya mashamba darasa yakuhamasisha matumizi ya mbolea na mbegu Bora, Kuzindua zoezi la ugawaji na upandaji wa Miche ya minazi, Kuzindua zoezi la ugawaji na upandaji wa mikorosho mipya, Pamoja na kukabidhi zawadi Kwa Wakulima washindi.
30/12/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa