Msimamizi wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi.Beatrice Mwinuka leo tarehe 26/09/2024 ametoa maelekezo muhimu kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao unatarajia kufanyika Nov 27,2024.
Aidha maelekezo hayo yamelenga Kutoa mwongozo ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa uwazi haki na usawa kwa kuzingatia sheria na taratibu za Uchaguzi zilizowekwa.
Akitoa maelekezo hayo kwenye kikao kifupi kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri hiyo uliopo mbuyuni Masasi ambacho kimewakutanisha kwa pamoja viongozi wa Vyama vya Siasa, viongozi wa dini, mamwenye, wazeee maarufu, wenyeviti kutoka vikundi vya Wanawake na Vijana, uongozi wa Kijiji na Kata ya Mbuyuni, wajumbe wa Kamati ya Uchaguzi, pamoja na Watumishi kutoka kada mbalimbali ngazi ya Halmashauri hiyo.
Amesema " leo Tanzania nzima tunatoa maelezo ya uchaguzi kwaiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi tumewaalika kwa ajili ya kusaidia maelezo haya Lakini pia kwenda kuhamasisha jamii yetu tumefanya uhamasishaji mbalimbali kwa kutumia vyombo vya habari, mitandao ya kijamii, Lakini nasi tuliopo hapa twende tukaieleze Jamii inayotuzunguka "
Amesema kikubwa anachozungumza leo akiwa ndiye msimamizi wa uchaguzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ni maelezo yakutoa ratiba nzima ya Zoezi litakalofanyika, maeneo ambayo watafanyia uchaguzi na nini ambacho kinatakiwa kufanyika kwenye zoezi hilo.
Bi.Mwinuka ameendelea kuelezea kuwa kwa mujibu wa Kanuni ya 9 kifungu (cha 1 -2) cha Kanuni ya uchaguzi wa mwenyekiti wa kijiji, kitongoji na Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji katika Mamlaka za Serikali za Mitaa Kwa mwaka 2024, msimamizi wa uchaguzi amepewa Mamlaka ya Kutoa maelekezo kuhusu uchaguzi, na maelekezo hayo yanatolewa siku 62 kabla ya uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha kuwa taratibu zote zinafuatwa na kwamba wapiga kura pamoja na wagombea wanapata taarifa zote zinazohitajika kwa wakati.
"Maelekezo haya pia yanafafanua hatua zinazoongoza mchakato wa uchaguzi kuanzia uandikishaji wapiga kura, uchukuaji na urejeshwaji wa fomu kwa wagombea, uteuzi wa wagombea na tarehe siku ya Uchaguzi."
Amesema kwa mujibu wa tangazo la uchaguzi lililotolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 4 ya Uchaguzi wa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa, tangazo linaeleza kwamba Uchaguzi huo utafanyika tarehe 27 Nov 2024, huku ikitanguliwa na zoezi la uandikishaji wapiga kura litakalofanyika tarehe 11-20 Oktoba 2024 katika vituo 886 vilivyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Akielezea zoezi la kuchukua na kurudisha fomu kwa wagombea Mwinuka amesema fomu za kugombea zitatolewa kuanzia tarehe 1-7 Nov 2024 kwa msimamizi msaidizi wa uchaguzi, huku zoez la uteuzi wa wagombea kwa mujibu wa Kanuni namba 18 uteuzi utafanyika tarehe 08 Nov 2024, wakati pingamizi dhidi ya uteuzi kwa mujibu wa Kanuni namba 23 ni kuanzia tarehe 8-9 Nov 2024 huku uamuzi wa pingamizi utatolewa tarehe 8-10 Nov 2024 .
"Rufaa dhidi ya uamuzi kuhusu pingamizi ya uteuzi zitapokelewa kuanzia Nov 10-13, 2024, ikiwa kampeni za Uchaguzi kwa mujibu wa Kanuni namba 27 zitaanza tarehe 20-26 Nov 2024 .
Hata hivyo msimamizi huyo wa uchaguzi Halmashauri ya Wilaya Masasi amehitimisha maelekezo yake kwa Kutoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kushiriki kikamilifu katika mchakato huo wa uchaguzi kuanzia hatua ya kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura ambayo ni hatua muhimu inayompa haki ya kushiriki katika uchaguzi kama mpiga kura au mgombea, hivyo Wananchi wamehimizwa kujitokeza kwa wingi kujiandikisha ili kutimiza haki yao ya kupiga kura au kugombea uongozi.
Nafasi zinazogombewa kwenye uchaguzi huo ni nafasi ya Mwenyekiti wa Kijiji, nafasi ya Mwenyekiti wa kitongoji, Wajumbe wa Halmashauri kundi mchanganyiko na wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji kundi la Wanawake.
26/09/2024
@.. Masasi DC
Kazi iendeleeee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa