Mbunge wa Jimbo la Ndanda Halmashauri ya Wilaya Masasi mhe.Cecil Mwambe ameiomba Serikali kuendelea kukiinua kituo Cha Afya Chiwale kwa kuboresha miundo mbinu mbalimbali ili kituo hicho kiweze kupandishwa hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya.
Mhe.Mwambe ametoa ombi hilo kwa mhe.Rais Dokta Samia Suluhu Hassan Lakini kupitia kwa Waziri wa Ulinzi na jeshi la Kujenga Taifa mhe.Stergomena Tax ambaye amekuwa mgeni rasmi Katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kituo Cha Mionzi kilichopo katika kituo Cha Afya Chiwale Halmashauri ya Wilaya Masasi.
Amesema Kata ya Chiwale mpaka Sasa kwenye Jimbo la Ndanda, ni Moja ya kata ambazo zimepokea fedha nyingi Sana za miradi ya Maendeleo, na hasa katika kipindi Cha uongozi wa mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, maendeleo ni makubwa sana na hivyo wao hawana budi kumuunga mkono na kumshukuru kwa mambo yote anayowafanyia.
Amesema " Miaka minne hadi mitano iliyopita kulikuwa na kero kubwa za miundo mbinu ya hospitali kwenye kituo Cha Afya Chiwale lakini Serikali kwa makusudi iliamua kutuletea X-ray baada ya mimi kupata nafasi ya kusema bungeni mbele ya bunge letu, Lakini pia alipofika mhe.Rais na hili nililisemea na lilibaki jukumu Moja tu la kupata Jengo"..alisema Mwambe
Ameendelea kuelezea kuwa anamshukuru sana mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi mhe.Ibrahimu Chiputula pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Bi.Beatrce Mwinuka kwa kuamua kutenga fedha kwa ajili ya Kujenga Jengo hilo ili kuweza kuunga mkono Maendeleo ya Wananchi wa Chiwale.
"Jengo hili linakuwa mkombozi mkubwa kwasababu huduma za Mionzi, X-ray zitakuwa zinapatikana hapa ukilinganisha na sasa Wananchi wamekuwa wakipata shida kubwa kulazimika kuzifuata huduma hizo katika maeneo mengine ili kupata matibabu".
Aidha mhe. Mwambe pamoja na kumshukuru mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia gari ya Wagonjwa ambalo limekuwa mkombozi mkubwa kwa Wananchi wa Chiwale, pia akatumia fursa hiyo kumuomba mhe.Waziri kumfikishia ombi lao mhe.Rais kwamba kituo Chao Cha Chiwale ni kikubwa sana na kinatoa huduma kwenye Kata zaidi ya 8 zilizopo upande wa magharibi, na pia kituo kinatumika kama sehemu ya rufaa.
"hivyo kutokana na hadhi yake tunakuomba Sana mhe.Waziri tuna tatizo la kuweza kukiinua kituo chetu Cha Chiwale kipate hadhi ya kuwa hospitali ili kiweze Kutoa huduma za kibingwa na bobezi hapo baadaye, kwasababu hapa tunakosa wodi ya akina baba, wodi ya upasuaji na wodi ya Watoto, hivyo miundo mbinu hii ikipatikana mara moja eneo hili litapandishwa hadhi.
13/11/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa