Baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa pamoja wameazimia mazao yote yanayolimwa katika ukanda wa Jimbo la Lulindi ambayo yapo kwenye mfumo wa stakabadhi ghalani, kuanzia sasa Mazao hayo yakusanywe kwenye ghala kuu la halmashauri hiyo ambalo lipo kwenye Kijiji Cha Chiungutwa kata ya Chiungutwa.
Katika kikao maalumu kilichofanyika tarehe 30/07/2024 waheshimiwa hao wamekubaliana kwa kauli moja kuwa kuelekea msimu wa mavuno ya mbaazi na mazao mengine yote yatakusanywa kwenye ghala kuu la Halmashauri.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Lauteri John Kanoni amewapongeza waheshimiwa Madiwani kwa uamuzi huo uliofanywa na baraza hilo huku pia akielezea kuwa naye ni muumini mkubwa wa ukusanyaji wa mapato ambayo ndio moyo wa Halmashauri hivyo hatua hiyo anaiunga mkono na anawaaidi kuwapa ushirikiano.
Hata hivyo mhe.Kanoni amehitimisha kwa kusema kuwa Halmashauri ni mamlaka inayojitegemea na inaendeshwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu hivyo kwa maamuzi hayo ya waheshimiwa madiwani ni halali na hayana ukakasi, zaidi ni kwenda kuyasimamia kulingana na baraza lilivyoazimia.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa