Kufuatia Agizo la Mhe. Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania , John Pombe Magufuli la tarehe 21 Mei, 2020 la kutaka vyuo vyote na wanafunzi wa kidato cha sita kufunguliwa kuanzia tarehe 1 Juni, 2020, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeanza kufanya maandalizi ya kufungua shule kwa wanafunzi wa kidato cha sita kwa kuhakikisha shule zote zinazingatia mambo muhimu kwa kuweka mazingira salama pindi watakapo kuwa shule muda wote.
wanafunzi hao wanatarajia kuanza mitihani yao tarehe 29 Juni, 2020.
Maandalizi hayo yanazingatia uwepo wa vitakasa mikono, uvaaji wa barakoa, uwepo wa nafasi maeneo ya madarasani, mabwenini, na katika mabwalo ya chakula ili kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Covid 19 unaosababishwa na virusi vya Corona.
akionge wakati wa ukaguzi wa mazingira ya shule pamoja na kukabidhi vifaa vya kutakasa mikono kwa shule 4 zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Masasi , Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri hiyo Dr. Miriamu Cheche aisistiza kuwa wanafunzi watapata elimu juu ya ugongwa huo ikiwa ni pamoja na namna ya kujikinga na kuwakinga wengine pindi wakiwa shuleni
Dr. Cheche aliongeza kuwa idara ya afya pia itahusika kutoa ushauri nasaa kwa wanafunzi ili kuwaondolea hofu itakayowasababisha wasisoma vizuri.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa