Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mhe. Selemani Mzee akitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi Agosti 3, 2019 yenye Kauli Mbiu "KILIMO, MIFUGO NA UVUVI KWA UKUAJI WA UCHUMI WA NCHI" Mkuu huyo wa wilaya aliwaasa washiriki wa maonesho hayo kutumia vizuri fursa hiyo kuzitangaza bizaa zao na kuziongezea thamani kwani kutachangia kuongezeka kwa Viwanda, ukuaji wa pato la Taifa na uchumi wa nchi yetu pamoja na ongezeko la ajira kupitia Kilimo. Hata hivyo aliendelea kwa kusema endapo pato la taifa litaongezeka kupitia kilimo kutamsaidia Mh. Raisi kuendelea kuboresha huduma mbalimbali za kijamii hapa nchini ikiwemo ujenzi wa reli nyingine ya kisasa kwa kanda ya kusini ambayo itakwenda mpaka mbinga reli hiyo inategemewa kujengwa na serikali katika nyakati zijazo.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya masasi Bi. Changwa Mkwazu kulia pamoja na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi Ndugu Festo Mwangalika kushoto wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye ufunguzi wa maonesho ya Nanenane 2019 yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi kwa kanda ya Kusini inayo jumuisha Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Wa kwanza kushoto ni Afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya masasi Ndugu Jeremiah Lubeleje,akifuatiwa na Afisa Utumishi Ndugu Festo Mwangalika, wa katikati ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi,Bi Changwa Mkwazu, na wa mwisho kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Masasi kwa pamoja wakionyesha ushiriki wao katika sherehe za uzinduzi wa maonesho ya Nanenane leo Agosti 3, 2019 katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi Kanda ya Kusini inayojumuisha Mikoa ya Lindi na Mtwara.
Picha upande wa kushoto ni Bibi Maarufu sana ndani ya Halmashauri ya wilaya ya masasi ambae ni mjasiliamali na mjuzi mzuri wa kutengeneza na kuuza vyungu vya asili
Mh. selemani mzee alipotembelea banda la vinyago na kujionea jinsi kazi hiyo ya sanaa inavyofanyika na kunufaisha wananchi kiuchumi
Hili ni moja kati ya eneo la Halmashauri ya wilaya ya masasi linaloonyesha kilimo cha mboga mboga ambazo zimelimwa kitaalamu na kisasa zaidi katika maonesho ya Nanenane Ngongo kanda ya kusini Mkoani Lindi.
Hiki ni kizimba kimojawapo cha Halmashauri ya wilaya ya masasi kinachoonyesha zao la Alizeti lililolimwa kitaalaamu katika maonyesho ya Nanenane Ngongo Mkoani Lindi 2019.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa