MAADHIMISHO HAYA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI YANATOA FURSA KILA
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe.Kassim Majaliwa Majaliwa (MB) amesema Serikali inatambua umuhimu wa kukuza Usawa wa Kijinsia na Uwezeshaji wa Wanawake kama njia mojawapo ya kukuza na kuimarisha Ustawi na hatmaye kufikia Maendeleo Jumuishi na endelevu kwa Jamii
Mhe.Majaliwa amesema hayo leo tarehe 06/03/2025 katika Kongamano la Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani Kanda ya Kusini yaliyofanyika katika Viwanja vya Maegesho Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya kuelekea katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ambayo yanatarajia kufanyika kitaifa jijini Arusha na mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Dkt.Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema lengo kubwa la Serikali ni kuhakikisha jamii ya Watanzania inaishi kwa umoja na mshikamano kati ya Wanawake na Wanaume na kwamba wote wawe wanapata huduma za msingi kwa haki na usawa katika nyanja zote ikiwemo huduma za kisheria, Elimu, Afya,uchumi na katika nafasi mbalimbali za maamuzi.
"Maadhimisho haya leo hii yanatoa fursa kila mmoja kujua haki yake ya msingi,kujua sisi sote ni sawa, lakini pia tunataka kuimarisha sekta ya uchumi kila mwanamke lazima awe na uwezo kiuchumi,je anapataje,aanze vipi,wapi, na nani anawezesha, hivyo wiki hii hutumia kwa wale wote wanaowezesha masuala ya kiuchumi kwa Wanawake wanajitokeza ili kutangaza fursa zao".
Aidha, mhe Majaliwa ameongeza kuwa ili kuendelea kuwawezesha Wanawake kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi, Serikali imeendelea kutoa fedha kupitia asilimia 10 ya mapato ya Halmashauri na kutoa mikopo hiyo kwa Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ambapo kupitia mikopo hiyo imewezesha makundi hayo na hasa Wanawake kutekeleza miradi kwa lengo la kuchangia ukuaji wa pato la mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
" Niwaombe Wanawake wote endeleeni kuhamasishana na kuunda vikundi vya ujasiriamali na mtumie fursa za uwepo wa madirisha yenye kutoa huduma za mikopo kwa Wanawake ili mjikwamue kiuchumi".
06/03/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa