"LISHE SIO KUJAZA TUMBO ZINGATIA UNACHOKULA"
Katika kutekeleza Afua mbalimbali za Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeweza kuhamasisha kufanya uchunguzi kwa watoto chini ya miaka mitano katika vituo mbalimbali vya kutolea huduma za Afya.
Katika uchunguzi huo umebaini kuwa Watoto waliokuwa na utapiamlo mkali ni 102 kwa kipindi cha mwaka 2023, hata hivyo watoto 98 wamepata matibabu ya utapiamlo mkali sawa na asilimia 96.1%, hata hivyo watoto hao wamepona kabisa.
Zahara Fundi ni Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Masasi akisoma taarifa ya Lishe kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava amesema huduma zingine ambazo zilitolewa ni Elimu ya Lishe kuhusu makundi sita ya chakula, chakula dawa na maziwa dawa kulingana na mahitaji na hali zao za Lishe.
Amesema kwa mwaka wa fedha kuanzia julai 2023 hadi April 2024 Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi 53,405,654.3/= ambapo kiasi cha shilingi 47,384594/= sawa na asilimia 88.73% kimetumika kwa ajili ya shughuli za lishe, lengo mpaka kufikia june 2024 Halmashauri iwe imetekeleza agizo la kutenga na kutoa shilingi 1000 kwa kila mtoto aliye chini ya miaka 5 kwa ajili ya kutekeleza shuguli mbalimbali za lishe.
Ameongeza kuwa halmashauri imeweza kufanya kaguzi za chumvi katika shule za msingi na jumla ya sampuli 163 zilipimwa na sampuli 113 ziligundulika kuwa na madini joto ya kutosha sawa na asilimia 63.3%.
Sambamba na hilo halmashauri imeweza kusimamia na kuhamasisha shule kutoa chakula na jumla ya shule za Sekondari na msingi zilizotoa chakula ni 173 sawa na asilimia 100%.
Pia halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeweza kuhamasisha wakina mama kuwapeleka watoto wao wenye umri wa (miezi 0- 59) kliniki ili kupima hali zao za lishe ambapo kuanzia April 2023 mpaka April 2024 jumla ya watoto 89,515 kati ya 90,371 sawa na asilimia 99.1% walipimwa hali zao za lishe pamoja na wazazi/ walezi kupewa unasihi wa ulishaji watoto (miezi 0-23) na wenye umri chini ya miaka mitano.
Hata hivyo mwenge wa uhuru baada ya taarifa hiyo umetembelea banda na kuona shughuli mbalimbali za lishe zinavyofanyika.
kazi iendelee!...
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa