Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava amekagua klabu ya wapinga rushwa katika shule ya Sekondari Ndanda huku akisaini cheti cha kuimarisha klabu hiyo.
Klabu hiyo ambayo lengo kuu la kuanzishwa kwake ni kutoa elimu juu ya kuzuia na kupambana na rushwa ilizinduliwa rasmi mnamo tarehe 17/09/2013 ikiwa ina jumla ya wanachama hai 160, mpaka sasa ina wanachama hai 120 ambao ni kidato cha tano, na ilikuwa na wanachama 142 kidato cha sita wamehitimu masomo yao tarehe 24/05/2024.
Akizungumza na wanafunzi hao, kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa 2024, ameanza kwa kuwapongeza wanafunzi hao " watoto wazuri sisi tunawashukuru sana, tunawapongeza hongereni mmechagua fungu jema kabisa kwa kujiunga na klabu hii, endeleeni kujifunza na suala lenu la masomo ya kawaida lakini pia endeleeni kujifunza na kukamata vizuri masuala haya ya mapambano dhidi ya rushwa kama ambavyo mnaendelea kufundishwa".alisema
Wakati huohuo ili kuendeleza uhifadhi wa mazingira katika eneo hilo mkimbiza mwenge wa uhuru kitaifa akaongoza wakimbiza mwenge wenzie kwa kupanda miti katika bustani maalumu ya viongozi mbalimbali wa kitaifa .
Kazi iendelee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa