KIKUNDI CHA VIJANA CHA TUINUANE _MANDIWA CHAPONGEZWA NA MWENGE WA UHURU 2024.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa 2024 Ndg.Godfrey Eliakimu Mzava amekipongeza kikundi cha Vijana cha Tuinuane kilichopo katika kijiji cha Mandiwa ambacho kinajihusisha na ufugaji wa Ng'ombe na uuzaji wa maziwa kwa kutoka kukaa tu mitaani na kujiunga kwenye kikundi na hatmaye wakachangamkia fursa ya mkopo kupitia asilimia 10 ya makusanyo ya Halmashauri kwenye mapato ya ndani.
Mzava ametoa pongezi hizo mara baada ya mbio za mwenge wa uhuru kutembelea, kuona na kukagua shughuli za ufugaji wa ng'ombe katika kikundi hicho ambapo ametumia fursa hiyo kueleza kuwa lengo la kupatiwa hizo fedha vijana ni kuwawezesha kufanya shughuli zao za kiuchumi na halmashauri ikitakiwa kuwalea, kuwaelekeza na baada ya kuwapatia fedha kuwafuatilia kuona kweli wanafanya hizo shughuli, wanazalisha,wanapata faida, je kuna tija kutokana na shguhuli wanazozifanya.
Pia ameongeza kuwa, Maafisa Mifugo na Maafisa maendeleo wanatakiwa nao kuwatembelea kuwapa miongozo mbalimbali na kuona wanapata faida na kama kuna changamoto zinawakabili wanapaswa kuwashauri utaalamu upi wanapaswa kuutumia.
Mwaka wa fedha 2021/2022 Halmashauri ya Wilaya yaMasasi iliwapatia mkopo wa shilingi 5,000,000/= kupitia fedha za asilimia 4% za mfuko wa Maendeleo ya vijana, na kwa mujibu wa taarifa ya kikundi hicho imeeleza kuwa marejesho ya mkopo huo yamefanyika kwa miaka 2 yaani 2,500, 000/= kila mwaka kuanzia mwaka 2021/2022 na kumalizia mwaka 2022/2023.
Taarifa inasema kupitia mkopo huo zipo faida kadhaa ambazo wanajivunia kama kikundi ikiwemo mkopo umewawezesha kikundi hicho kujenga banda na kununua ng'ombe wawili (2) wa maziwa ambapo hadi sasa tayari kuna ongezeko la Ng'ombe 4, upatikanaji wa maziwa umeongeza uboreshaji wa lishe kwa jamii inayowazunguka, ongezeko la kipato kwa wanakikundi sanjari na kuimarisha umoja baina ya wanakikundi.
Hata hivyo matarajio ya kikundi ni kuongeza ng'ombe wengine na kutoa ajira kwa vijana wengine kupitia mradi huo wa ufugaji wa ng'ombe wa maziwa.
Hata hivyo kikundi cha vijana tuinuane Mandiwa kina jumla ya wanachama 6, watano wanawake na mwanaume mmoja ,kilianza rasmi tarehe 01/07/2019 kikiwa na Ngombe mmoja wa maziwa pamoja na ujenzi wa banda ambazo zilitokana na michango ya wanakikundi yenye thamani ya tshs.2,499,975.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa