Bw.Innocent Dwasi ni Afisa kilimo, pia ni mtaalamu wa Afya ya udongo akitoa maelekezo ya namna kifaa maalumu Cha kupimia udongo kinavyofanya kazi (soil scanner) kwa Bi.Aziza Kabwe ambaye ni Mfamasia kutoka Halmashauri ya Wilaya Masasi .
Kazi kubwa ya kifaa hicho ni kuwezesha kutambua hali halisi ya udongo, mapungufu ya udongo na mahitaji ya udongo ili kuboresha Afya ya udongo huo.
Ifahamike kwamba udongo usio na afya maana yake ni udongo mfu,ili kurudishia uhai udongo huo mkulima anahitajika kuongeza virutubisho mbalimbali ikiwemo naitrojen, potasiyamu na phosphorasi. Hivi ni virutubisho muhimu katika udongo ambavyo vinasaidia mmea kukua vizuri.
Hata hivyo vipo virutubisho vingine ambavyo huchangamsha udongo kwa Kutoa nafasi ya viumbe mbalimbali kumeng'enya udongo na kuruhusu uwepo wa viumbe vingi rafiki wa udongo na mimea mbalimbali ambayo kwa pamoja huchangia uwepo wa bioanual.
Hayo yamefanyika Jana Tarehe 08/08/2024 katika kilele Cha maadhimisho ya nane nane kanda ya kusini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Ngongo -Lindi.
09/08/2024
@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa