Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara mapema tarehe 04 march - 05, 2025 imefanya Ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi.
Kamati hiyo ambayo imeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Masasi Bi.Mariam Kasembe, ikiwa katika Jimbo la Lulindi imefanikiwa kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Maparawe ambapo kwasasa mradi huo unatoa huduma za Wagonjwa wa nje, huduma za Uzazi na Uzazi wa mpango pamoja na Maabara, ambazo kwa ujumla wake zimesaidia kupunguza idadi ya akina mama wanaojifungulia nyumbani, zimeongeza idadi ya akina mama wanaoanza kliniki kwa wakati na huku ikiongeza idadi ya watoto wanaopata chanjo kwani hapo awali ilikuwa vigumu kutokana na umbali wa kufuata huduma hizo.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mradi huo ambayo imesomwa mbele ya Kamati hiyo imeeleza kwamba katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/ 2024 Kijiji cha Maparawe kilipokea fedha za ruzuku za Maendeleo kutoka Serikali kuu zenye jumla ya sh.Milioni 50 ambazo zilitumika kukamilisha Zahanati hiyo ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zilizoonyeshwa na Wananchi wa Maparawe hasa kwenye kujitolea katika shughuli za Maendeleo.
Hata hivyo mnamo tarehe 09/10/2024 mhe.Stergomena L.Tax Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa aliweka jiwe la Msingi kwenye Zahanati hiyo ambayo inatumika.
"Hata hivyo baada ya Halmashauri kuridhishwa na utekelezaji wa Mradi huu, waliongeza jumla ya sh.milioni 16,750,000.00 ambazo had sasa sh.milioni 16,050,000.00 zimetumika na sh.700,000.00 zimebaki kwenye akaunti.Fedha hizi zinatumika kujenga kichomea taka, vyoo matundu 2 ya Watumishi, mfumo wa maji, matundu 3 ya vyoo vya Wagonjwa, Ununuzi wa Samani pamoja na ujenzi wa shimo la kondo la nyuma."
Pia ifahamike kuwa mhe.Waziri wa Ulinzi aliwapatia jumla ya sh.Milioni 2,000,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la kupumzikia Wagonjwa ambalo hadi sasa vifaa vyote vimeshanunuliwa .
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Masasi Bi.Mariam Kasembe pamoja na kuwaomba Wananchi wa Maparawe kuendelea kuitunza Zahanati hiyo pia ameendelea kuwapongeza Wananchi wote wa Maparawe kwa kujitoa kikamilifu kushirikiana na Serikali katika kujenga Zahanati hiyo ambayo imekuwa na manufaa makubwa na mkombozi kwao.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa