Kamati ya Fedha, Uongozi Na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara Leo tarehe 06/05/2025 imefanya Ziara ya kutembelea na kukagua Miradi mbalimbali ya Maendeleo ambayo inatekelezwa katika Halmashauri hiyo.
Kamati hiyo Chini ya Mwenyekiti wake mhe.Ibrahimu Chiputula ambaye pia ni Diwani wa kata ya Mpeta, imejumuisha baadhi ya Waheshimiwa ambao ni wajumbe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Ndg.Alphaxard Etanga pamoja na Wakuu wa Idara na Vitengo.
Katika Jimbo la Lulindi Kamati hiyo imetembelea na Kukagua Mradi wa Umaliziaji wa Miundombinu ya Hospitali ya Wilaya ya Masasi iliopo katika kijiji cha Mbuyuni ambapo mnamo tarehe 03/12/2024 Halmashauri ilipokea fedha Shilingi Milioni 176 (176,000,000.00) kutoka Serikali kuu kwa ajili ya Umaliziaji wa Miundombinu ya Hospitali ikiwemo Jengo la Upasuaji mkubwa, Wodi mbili za upasuaji (ME&KE) Jengo la kuhifadhia Maiti, Jengo la Kichomea taka pamoja na ukarabati wa baadhi ya majengo yaliyokuwepo tangu awali.
Akizungumza mbele ya Kamati hiyo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Dkt.Ruben Mwakilima amesema mpaka sasa kazi zilizofanyika ni Ukamilishaji wa mfumo wa umeme, mfumo wa maji safi na taka, Ukamilishaji wa rangi nje na ndani ya majengo, uwekaji wa vioo vya aluminium, uwekaji wa sakafu ya Epoxy, Ujengaji wa sluice sinks na uwekaji wa Viyoyozi.
" Pamoja na hatua hii lakini kazi zilizobaki kukamilisha Mradi ni uwekaji milango ya ndani kazi ambayo inaendelea kwasasa, uwekaji wa vents na ukamilishaji wa ujenzi wa mashimo ya maji taka"..alisema Mwakilima
Majengo yaliyokarabatiwa ni Jengo la utawala, Jengo la Kufulia na Jengo la Wodi ya Watoto ambapo ukarabati wake umehusisha zaidi upakaji rangi na mifumo ya maji safi na taka.
Hata hivyo kazi zilizofanyika zimegharimu kiasi cha Shilingi Milioni 123,765,410 hivyo kiasi kilichobaki ni Shilingi Milioni 52,234,600.
06/05 /2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa