Mananchi wa Halmashauri ya wilaya ya masasi mkoani mtwara wapatiwa mafunzo yanayolenga ushirikishwaji wa jamii katika kuleta maendeleo ya kielimu katika vijiji vyao ili kuwezesha jamii kuwajibika katika kuboresha elimu ikiwemo kushiriki kujenga miundombinu ya shule, kuhimiza watoto kuhudhuria shuleni na mambo mengine.
Mafunzo hayo yametolewa Kupitia mradi wa USAID Tusome pamoja ikishirikiana na serikali katika mkoa wa mtwara , kutoa mafunzo hayo ya mpango jamii wa uhamasishaji na utekelezaji elimu (MJUUE) wenye lengo la kuhamasisha jamii katika kubaini changamoto katika sekta ya elimu zinazo athiri ubora wa elimu na ufaulu, Kubaini rasilimali na utatuzi wa changamoto hizo.
Akiongea wakati wa kupokea mipango kazi iliyoandaliwa na wawakilishi wa jamii kutoka kila kijiji Afisa Elimu Takwimu wa halmashauri ya wilaya ya masasi alisema kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuamsha ari kwa wananchi ya kuona suala la elimu ni la watu wote na sio la serikali na walimu tu.
“ Wananchi wengi wamekuwa na kasumba kuwa suala la kusimamia elimu ni la serikali na walimu pekee na hilo limepelekea uboa wa elimu kushuka na miundombinu kuwa mibovu lakini kwa mafunzo haya tunategemea jamii itahusika moja kwa moja katika kuboresha elimu” alisema Tatu
Tatu alisema kuwa Kupitia mafunzo hayo jamii sasa imejengewa uwezo wa kutambua kuwa wao kama jamii wana wajibu wa kusimamia na kuendeleza shule zilizopo katika vijiji vyao ikiwemo kujitolea kutekeleza miradi ya ujenzi katika shule na kujitolea kama jamii kuboresha shule yao badala ya kusubiri serikali ifanye kila kitu.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa