Kamati ya Siasa mkoa wa Mtwara ikiongozwa na Mwenyekiti wa Ccm mkoa Saidi Nyengedi pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala katika kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama Chama Mapinduzi imetembelea na kukagua ujenzi wa Nyumba ya walimu 2 in 1 inayojengwa katika Shule ya Sekondari mitesa Halmashauri Ya Wilaya Ya Masasi.
Kamati hiyo imeonyesha kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo ambao utekelezaji wake umeendana Kabisa na thamani ya fedha zilizotumika.
Hata hivyo kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa mradi huo unaogharimu kiasi cha shilingi Milioni 95, unatekelezwa kwa njia ya force account hadi sasa umefikia hatua ya upauaji na Shughuli za ukamilishaji zinaendelea.
Taarifa hiyo imeeleza kwamba mnamo tarehe 29 /06/2024 shule ilipokea kiasi cha shilingi Milioni 95 Kutoka Serikali kuu kupitia fedha za wahisani na mradi wa Sequip kwa ujenzi wa Nyumba 1 ya walimu (2 in 1) sambamba na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundisha kwa walimu.
Hata hivyo mradi ulutakiwa kutekelezwa ndani ya siku 90 kuanzia tarehe 01/07/2024 - 30/09/2024 ila kwakuwa wakati zinaingizwa fedha hizo ilikuwa ni kipindi cha mwisho wa mwaka wa Serikali na fedha hizo zilianza kutumika kwa bakaa ya fedha Mwaka 2023/2024 kwenye bajeti ya mwaka 2024/2025, hivyo utekelezaji rasmi wa mradi ulianza tarehe 20/08/2024 ambapo hadi sasa kiasi kilichotumika ni shilingi milioni 61,820,382.00 na kiasi kilichobaki ni shilingi 33,179,618.00 na kinaendelea kutumika.
Aidha katika kipindi Cha utekelezaji mradi ulipitia changamoto ya ukosefu wa maji pamoja na changamoto ya mfumo wa manunuzi wa kielektroniki wa NeST lakini kwa kushirikiana na Wataalamu na Viongozi waliweza kutatua changamoto hizo na kuwezesha mradi kufikia hatua hiyo.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Ndg Said Nyengedi pamoja Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Kenani Sawala wametumia wasaa huo kumshukuru mheshimiwa Rais Dokta Samia Suluhu Hassan Kwa kuendelea kuupatia Mkoa wa Mtwara Fedha Kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo inaleta maendeleo makubwa ndani ya Mkoa mzima wa Mtwara.
08/01/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa