Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara kwa kupata HATI SAFI katika ukaguzi wa Hesabu za Halmashauri hiyo zilizoishia tarehe 30 mwezi juni, 2017 kutokana na kutumika vyema fedha za serikali kwa kuzingatia kanuni na taratibu za matumizi ya fedha hizo.
Wajumbe wakiwa kwenye Mkutano maalumu wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakati wa kupokea na kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo tarehe 17.07.2018 katika ukumbi wa Halmashauri
Wakati wa ukaguzi huo wa fedha kwa mwaka wa fedha 2016/2017, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ilipata hoja 71 lakini iliweza kujibu vizuri jumla ya hoja 54 na hatimaye kufutwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali baada ya kuridhika na majibu.
Mheshimiwa Diwani wa kata ya Mijelejele Juma Pole akichangia wakati wa kujadili na kupokea taarifa ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo tarehe 17.07.2018 katika ukumbi wa Halmashauri
Pongezi hizo zimetolewa leo na mwakilishi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Mtwara ndugu Ibrahim Ndendemi wakati akiwasilisha taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Halmashauri hiyo katika mkutano maalumu wa baraza la Madiwani la kujadili hoja za ukaguzi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na hoja za nyuma na kueleza kuwa halimashauri iliweza kufanya utekelezaji wa shughuli zake kwa kufuata taratibu na sheria za matumizi ya fedha za umma.
waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi wakifuatilia mjadala wakati wa kujadili na kupokea taarifa ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali leo tarehe 17.07.2018 katika ukumbi wa Halmashauri
Ndendemi alilieleza baraza kuwa pamoja na Halmashauri kupata hati safi, wakati wa ukaguzi baadhi ya dosari/ mapungufu yalibainika ambapo Halmashauri ilihojiwa jumla ya hoja 71 na hoja 54 zilijibiwa vizuri na kufutwa huku hoja 19 zikiwa bado hazijajibiwa hivyo halmashauri izingatie ushauri wa Mkaguzi ili halmashauri isiwe na hoja kabisa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe. Gelasius Byakanwa ameeleza kuwa siri kubwa ya halmashauri kwa Mkoa wa Mtwara kupata hati safi ni kutokana na usimamizi mzuri wa mkoa lakini pia watendaji wa Halmashauri kufanya kazi kwa weledi unaozingatia sheria na kanuni za matumizi ya fedha za umma ikiwemo sheria ya manunuzi ya umma.
Ili kuondokana na hoja za madeni, Byakanwa ameishauri Halmashauri kubuni vyanzo vipya vya mapato lengo ikiwa ni kukusanya mapato kwa kiasi kikubwa na hatimaye kulipa madeni na kuiwezesha halmashauri kutekeleza shughuli zingine za maendeleo.
Akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa Hesabu za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa mwaka wa fedha ulioishia mwezi juni 2017, kwenye Mkutano Maalumu wa Baraza la Madiwani Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Changwa M. Mkwazu alisema, kwa mwaka wa fedha 2016 /2017 Halmashauri ilihojiwa jumla ya hoja 19 ambapo hoja 8 zimafungwa 11 hazijafungwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi bibi Changwa M. Mkwazu akiwasilisha taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia 2017 leo tarehe 17.07.2018 katika ukumbi wa Halmashauri
Ukaguzi wa fedha za katika mamlaka za serikali za mitaa unafanyika kwa mujibu wa sheria ya fedha ya usimamizi wa fedha ya mwaka 1997 na marekebisho yake ya mwaka 2009
Mweka Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Said Lihyuka akiwasilisha Hoja zilizohojiwa na wakaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia 2017 leo tarehe 17.07.2018 katika ukumbi wa Halmashauri
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa