HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI YAPITISHA BAJETI 31,147,557,341.00 KWA MWAKA WA FEDHA 2017/2018 KWA AJILI YA SHUGHULI ZA MAENDELEO
Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imepitisha bajeti ya Ths. 31,147,557,341.00 kwa Mwaka wa fedha wa 2017/2018 kutoka vyanzo mbalimbali vya Halmashauri kati ya fedha hizo Tshs.4,173,696,000.00 zitatokana na mapato ya Ndani na Ruzuku toka Serikali Kuu Tshs.26,973,963,341.00 kwa ajili ya Mishahara, Matumizi mengineyo na Miradi ya Maendeleo.
Akiwasilisha bajeti hiyo katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya masasi siku ya tarehe 18.01.2017 kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji(H/W) Masasi, Bw. Jeremiah Lubeleje amesema kwa upande wa Mapato ya Ndani,Halmashauri imejipanga kukusanya jumla ya Tshs. 4,173,696,000.00 kutoka vyanzo vyake vya mapato ambapo ongezeko hili la makusanyo ya ndani ni asilimia 4.27 ukilinganisha na makisio ya mwaka 2016/2017.
Lubeleje alisema kuwa halmashauri ya wilaya ya masasi katika makusanyo yake ya ndani inatarajia kukusanya shilingi bilioni 2,076,125,000.00 kupitia chanzo cha ushuru wa mazao ambapo katika kiasi hicho ushuru wa korosho pekee Halmashauri inategemewa kukusanya jumla ya Tsh bilioni 1,430,000,000.00
Bajeti hiyo imeandaliwa kwa kuzingatia vipaumbele vya Serikali ya Awamu ya Tano, Sheria ya Bajeti ya mwaka 2015 namba 11,Mpango wa maendeleo wa miaka mitano 2015/2016 – 2010/2021 na Miongozo mingine ya kitaifa, kimkoa na kiwilaya ikiwa na lengo la kuwatumikia wananchi na kuwaletea maendeleo wananchi wa Masasi.
Bw. Lubeleje alisema bajeti ya mwaka 2017/2018 imejikita zaidi katika kuhakikisha miradi viporo inakamilika ikiwa ni pamoja na kutekeleza miradi inayoendelea na kuiwekea fedha kwa mwaka 2017/2018.
Pia Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imepania kutenga fedha 60% za mapato ya ndani kwa ajili ya miradi ya maendeleo na 40% itatumika kwa ajili ya matumizi mengineyo sambamba na hilo imeelekezwa kuwa 40% ya fedha za mapato zinazotokana na kilimo zikatumike kwenye Idara husika kwa 20% kilimo,15% Mifugo na 5% Uvuvi.
Hata hivyo Halmashauri katika kutekeleza maagizo ya kuzifanya shule za Chidya na Ndwika kuwa Sekondari za Kidato cha 5&6 imepanga kuboresha miundombinu ili kufanikisha jambo hilo sambamba na kuimarisha na kuongeza mahudhurio na ufaulu imepanga kusaidia chakula mashuleni.
Pamoja na bajeti hii, Halmashauri imepata changamoto kadhaa wakati wa kutekeleza bajeti ya mwaka 2016/2017 ikiwa ni pamoja na fedha kutoka Serikali kuu kupokelewa kiasi kidogo, kuchelewa kupokelewa fedha au kutoletwa kwa wakati, michango midogo ya jamii sanjari na ukosefu wa usafiri wa uhakika baada ya Halmashauri kuchomewa magari yake tarehe 26.01.2013.
Alisema ufumbuzi wa changamoto hizo ni pamoja na kuongeza ukusanyaji wa mapato, jamii kuhamasishwa ili kuongeza moyo wa kujitolea kwa Halmashauri kuweka utaratibu wa kusaidia maeneo yale ambayo yameonesha moyo kujitolea ili wengine waweze kuiga tabia ya kujitolea ikiwa ni pamoja na kuweka bajeti ya ununuzi wa gari la kukusanyia mapato.
Baraza hilo la Madiwani liliidhinisha jumla ya Tshs. 31,147,559,341/= ambapo kati ya fedha hizo kamati ya Fedha Utawala na Mipango inategemea kukusanya na kutumia Tshs. 4,096,950,020/=, Kamati ya Ujenzi, Uchumi na Mazingira Tsh. 4,161,481,600/=, Kamati ya Elimu,Afya na Maji Tshs. 22,859,127,721/= na Kamati ya kudhibiti UKIMWI jumla ya Tshs. 30,000,000/=.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa