Benki ya CRDB Kanda ya kusini Leo tarehe 19/09/2024 imefanya kikao na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya Masasi huku wakisisitizwa kununua hisa za benki ya CRDB ili kuongeza makadirio ya mapato.
Kikao hicho kilichofanyika Katika ukumbi mdogo wa Halmashauri hiyo Mbuyuni Masasi pamoja na mambo mengine kimewashirikisha wakuu hao wa idara na vitengo mbalimbali, huku wawezeshaji Wakuu wakiwa ni wawakilishi Kutoka Benki ya CRDB Kanda ya kusini.
Bw. Emmanuel Biganio ni Meneja biashara wa benki ya CRDB Kanda ya kusini amesema kwamba anatambua kazi kubwa ya Halmashauri ni kutengeneza vyanzo vipya vya mapato ambavyo havina mgogoro na wananchi na vinafuata taratibu na sheria, hivyo fursa moja wapo "niwaombe kwenye mipango yenu ya Maendeleo mfikirie kununua hisa za benki ya CRDB ambayo ni njia nzuri itakayowasaidia kujipambanua zaidi kama taasisi na kuongeza makadirio ya mapato.
Amesema " kipaumbele chenu nyie kama wataalamu ni Kuleta maendeleo ili wananchi waishi vizuri nyakati zote, japo kuna sehemu kubwa ya upotevu wa mapato hasusani Katika maeneo ya kutolea huduma kama hospitali na maeneo mengine hivyo niwaombe katika sehemu zile zenye makusanyo mazuri mtuambie ili kama benki tusaidie kukusanya kwenye hayo maeneo.
19/09/2024
Kazi iendeleeee!
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa