Fahamu makundi sita ya vyakula.
Afisa lishe kutoka halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi.Irene Shaban ametoa elimu ya lishe pamoja na Elimu ya Unyonyeshaji kwa wananchi mbalimbali ambao walijitokeza kupata huduma hizo kwenye banda lao la maonesho ya nane nane ambayo yamefanyika Ngongo Lindi na kufungwa rasmi Jana tarehe 08/08/2024 na Waziri wa nchi, ofisi ya Rais,Ikulu (kazi maalumu) Mhe.kapt.George Huruma Mkuchika.
Elimu ya Lishe pamoja na Elimu ya Unyonyeshaji Ilitolewa , kadhalika na Upimaji wa Uzito kwa Urefu ili kujua Hali ya Lishe ulifanyika
Elimu ya Lishe Ilitolewa Kuhusu Lishe na mlo kamili pamoja na Makundi sita ya chakula yalielezwa .
Makundi sita ya chakula ni
1. Nafaka mizizi yenye wanga na ndizi za kupika: huupatia mwili nguvu/ Nishati
2. Mbogamboga : huupatia mwili Vitamini pamoja na madini
3. Matunda: huupatia mwili vitamin pamoja na madini
4. Jamii ya kunde , karanga na mbegu za mafuta: kundi hili huupatia mwili protini pamoja na kulinda Kinga ya mwili
5. Vyakula vyenye asili ya wanyama huupatia mwili protini
6. Mafuta ( yenye asili ya mimea pamoja na wanyama) ambayo ni salama kwa Afya: kundi hili hulinda viungo muhimu vya mwili kama vile Figo na moyo
Kadhalika Elimu ya Unyonyeshaji Ilitolewa Kuhusu
- Umuhimu wa Maziwa ya mama kwa mama pamoja na mtoto
- Kwa mtoto humsaidia kukua kiafya ,kiakili pamoja na kimwili , kadhalika Maziwa ya mama huimarisha uhusiano mzuri kati ya mama pamoja na mtoto .
Hivyo tunasisitiza wakina mama wote waliojifungua kunyonyesha Watoto wao Maziwa ya mama pekee ndani ya miezi 6 ya mwanzo bila kuwapatia kitu chochote na baada ya miezi 6 Watoto wataanzishiwa Chakula mbadala huku wakiendelea kunyonya Maziwa ya mama.
Hivo tunazidi kusisitiza kula mlo kamili kwa kuzingatia makundi sita ya chakula pia chakula kiwe kwa kiasi.
08/08/2024
@.. Masasi DC
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa