• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DCC MASASI: YARIDHIA PENDEKEZO LA KUBADILISHWA JINA LA TARAFA YA LISEKESE KUWA JINA JIPYA LA TARAFA YA LUKULEDI NA MAKAO MAKUU YAKE NI KATA YA CHIWALE.

Posted on: November 19th, 2024

Kamati ya Ushauri Wilaya (DCC) Wilayani Masasi Mkoani Mtwara leo tarehe 19/11/2024 imeketi na kuridhia kwa pamoja pendekezo la kubadilishwa Jina la tarafa ya Lisekese, kuwa sasa Jina jipya ni tarafa ya Lukuledi na makao makuu yake ni Kata ya Chiwale.


Kamati hiyo ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mkuu wa Wilaya ya Masasi mhe.Lauter Kanoni imefikia maamuzi hayo baada ya kufanyika kwa vikao mbalimbali vya maamuzi vilivyofanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na kikao cha Maendeleo ya tarafa Cha tarehe 19/08/2024 ambacho kilipendekeza ujenzi wa Ofisi na nyumba ya Afisa tarafa ijengwe katika Kata ya Chiwale kwa kuwa pamependekezwa kuwa makao makuu ya Tarafa ya Lukuledi.

Awali akisoma taarifa ya mapendekezo ya kubadilisha Jina la Tarafa ya Lisekese na kupitisha makao makuu ya Tarafa hiyo Bi. Irene Mbwana ambaye ndiye Afisa tarafa ya Lukuledi (awali ilikuwa Lisekese)  ameelezea kuwa kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya Mwaka 2022, Kata yenye watu wengi ni Kata ya Chiwale yenye jumla ya watu wapatao 21,466 na Kata yenye watu wachache ni Kata ya Chikunja yenye Jumla ya watu 6,423.


Amesema kwamba pamoja na Shughuli kuu za kiuchumi ni Kilimo cha mazao biashara Kama korosho, ufuta, mbaazi, na mazao ya chakula Kama vile mahindi na muhogo huku baadhi ya Wananchi wakijishughulisha na biashara ndogo ndogo, pia sababu Nyingine ya pendekezo hilo ni kutokana na jiografia ya Kata ya Chiwale ambayo ipo katikati ya Kata zote 8 zilizopo katika Tarafa hiyo na inafikika kwa urahisi kutokea katika Kata zote.

"Kata ya Chiwale pia ina eneo la kutosha lenye uwezo wa kuruhusu ujenzi wa majengo mbalimbali ya Serikali Kama vile Ofisi ya Tarafa, Mahakama,nyumba ya Afisa tarafa, soko na kituo Cha polisi hivyo kubadilisha Jina la tarafa ya Lisekese kuwa Tarafa ya Lukuledi, tufahamu kuwa Tarafa ya Lisekese haina kijiji Wala Kata inayobeba Jina la tarafa ya Lisekese Kama ilivyo kwenye tarafa zinginge kama Lulindi, Chiungutwa na Machauru".


Kwa upande wao baadhi ya wajumbe walioshiriki kwenye kikao hicho cha Kamati hiyo ya  Ushauri Wilaya (DCC) wamepongeza hatua hiyo waliyofikia ya maelewano katika maeneo ya utawala ambapo wamejadiliana kwa amani na mwisho wa siku wametoka na wazo Moja ambalo linaendelea  kuweka historia kwa Jamii hususani kutumika Jina la tarafa ya Lukuledi kwasababu kwenye Kata ya lukuledi upo mto ambao unapakana na Wilaya ya Nachingwea na Masasi hivyo kuitwa Tarafa ya Lukuledi ni heshima kwako.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo ilipokea pia taarifa ya mrejesho wa Kitongoji cha Singino kilichoomba kuhamishiwa katika Kijiji Cha chikundi kutoka Katika Kijiji Cha Msigalila.

Kwa vipindi tofauti tofauti vikao mbalimbali vya kisheria vilikaa na kujadili ambapo kikao cha Tarehe 18/04/2023 kiliridhia ombi la kitongoji Cha Singino kuhamia katika Kijiji Cha Chikundi na kikao cha Maendeleo ya Kata (WDC) ya Kata ya Chikundi cha tarehe 23/05/2023 kwenye ajenda Na.02/MAY/WDC/2023 iliridhia ombi la kitongoji Cha Singino kutoka Kijiji Cha Msigalila kwenda Kijiji Cha Chikundi.


Hata hivyo Kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na.796 lililotolewa kwenye gazeti la Serikali Na 32/VOL.105 la tarehe 06/09/2024 Kutoka OR-TAMISEMI iliridhia maombi ya kitongoji Cha Singino kuhama Kutoka Kijiji Cha Msigalila kwenda Kijiji Cha Chikundi katika Kata ya Chikundi.


19/11/2024

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa