TAARIFA KWA UMMA.
Imeandaliwa na :
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara siku ya tarehe 08/02/2025 umepitisha Rasimu ya Mpango na Bajeti ya Tshs.47,850,929,593.00 inayotarajiwa Kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 ambayo ni sawa na ongezeko la asilimia 10.3 na Mapato ya ndani yameongezeka kwa asilimia 16.8 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.
Kati ya Fedha hizo Tshs.6,873,357,613.00 ni ruzuku ya Miradi ya Maendeleo kutoka Serikali kuu, Tshs. 4,880,595,000.00 ni fedha kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo kutoka kwa Wahisani, Tshs. 26,478,522,000.00 ni fedha kwa ajili ya malipo ya Mishahara ya Watumishi.
Kiasi cha Tshs. 6,915,174,980.00 fedha kutoka Mapato ya ndani kwa ajili ya Miradi na Matumizi mengineyo (OC PROPER).
Hata hivyo kulingana na Mwongozo uliotolewa , Vipaumbele vya Halmashauri kwa Mwaka 2025/2026 ni pamoja na kuanzisha na kuendeleza Miradi ya kimkakati kwa ajili ya kuongeza Mapato ya Halmashauri kwa Ujenzi wa ghala la mazao
mchanganyiko katika kata ya Chigugu na Chiungutwa.
Kuimarisha Usafirishaji wa vifaa na malighafi kwenye Miradi ya Maendeleo kwa kununua Lori moja(1).
Kuboresha huduma za Mawasiliano na Jamii kwa kuanzisha Redio ya Jamii.
Kuimarisha ulinzi na Usalama wa Raia na mali zao kwa kujenga Vituo 2 vya Polisi katika Kata za Chiwale na Mbuyuni.
Kukamilisha ujenzi wa vituo vya Afya 2 (Chikundi na Chikoropola) na Zahanati 2 katika Vijiji vya Mbangala na Liloya.
Kuanzisha na kuendeleza Miradi ya kimkakati kwa kujenga / kuboresha stendi ya Mabasi/ Hiace katika kata za Mbuyuni na Ndanda.
Kukamilisha vyumba vya Madarasa 56, nyumba 3 za walimu na vyumba 4 vya maabara.
Kipaumbele cha nane, katika kupunguza uhaba wa watumishi kwa kuajiri watumishi wapya 604 kwa kada za Afya 175, Elimu Msingi 214, Elimu Sekondari 76, Wahasibu wasaidizi 3, Kilimo 12, Mifugo 7, Ujenzi 3 na Utawala 43. Uhaba huu wa watumishi umetokana na kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma kama vile Shule na Zahanati na watumishi wengine kustaafu utumishi wa Umma.
09/02/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa