Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa niaba ya wananchi, limempongeza Mhe Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa maamuzi yake ya kununua korosho za wakulima kwa bei ya shilingi 3,300 baada ya minada ya kuuza zao hilo kusuasua.
“Sisi kama Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kwa niaba ya wananachi wetu, tunachukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kwa maamuzi yake ya kulinusuru zao la korosho kutokana na wafanyabiashara kuwa wababaishaji kwa kutaka kununua kwa bei ndogo ambayo haikuwa na maslahi kwa wakulima” alisema Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhe. Jumah Satmah.
Baraza la Madiwani limeahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi walioteuliwa kusimamia zoezi hilo kwa kuwahamasisha wakulima kupeleka korosho maghalani kwa sababu uhakika wa korosho zao kununuliwa kwa bei nzuri upo kwani hapo awali wakulima walisita kupeleka korosho maghalani kwa kuhofia kununuliwa kwa bei ndogo.
Tamko hilo la kumpongeza Mheshimiwa Rais limetolewa jana Tarehe 21.11.2018 kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani kujadili na kupitisha taarifa za utekelezaji kwa robo ya kwanza ya Julai hadi Septemba kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa