Mkutano wa Robo ya Nne 2018/2019 wa Baraza la Madiwani katika Halmashauri ya Wilayani Masasi umehitimishwa mapema leo katika Ukumbi wa Halmashauri. Katika Mkutano huo, Taarifa za Kata 34 za Halmashauri ya Wilaya ya masasi ambazo ni Mbuyuni, Chikoropola, Namajani, Mpindimbi, Ndanda, Chiwale,Chigugu,Chikukwe,Chikunja,Chiungutwa,Chiwata,Lipumbulu,Lulindi,Makong'onda,Lupaso,Mchauru,Mijelejele,Mitesa,Mkululu,Mkundi,Mlingula,Mpanyani,Mnavira,Mpeta,Msikisi,Mwena,Namalenga,Namatutwe, Nanganga,Nangoo,Nanjota,Sindano, zimejadiliwa kwa kina pamoja na wataalamu wa idara na vitengo mbalimbali ndani ya Halmashauri ya wilaya ya masasi pamoja na Taasisi nyingine kama vile Takukuru,Tarura,Nida,Makampuni ya simu ikiwemo Tigo,Vodacom,TTCL,Meneja wa Bima mkoa,Bila kusahau Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya kwa ajili ya kujibu hoja mbalimbali za waheshimiwa madiwani kwa niaba ya wananchi kwa ujumla.Ambapo waheshimiwa madiwani waliweza kuhoji maswala mbalimbali yanayohusu wananchi wao likiwemo tatizo la Mimba mashuleni,uhaba wa watumishi hasa katika Idara ya Mifugo,pamoja na Huduma ya Bima ya Afya kwa wananchi yaani CHF Iliyoboreshwa ambapo Meneja wa Bima Mkoa aliwaeleza waheshimiwa madiwani kuwa wana mpango wa kuzindua Huduma mpya ya Bima ijulikanayo kama Mafao ya Vifurushi vya Bima kwa wananchi ikiwa huduma hiyo itampa fursa mwananchi mojamoja kuweza kulipia huduma ya Bima kadili unavyoweza.Huduma hii itazinduliwa kuanzia tarehe1/09/2019 na kuwataka wananchi wawe tayari kuipokea huduma hiyo.
Hata hinyo Baraza hilo leo lilihitimishwa kwa kufanya uchaguzi wa kuwachagua viongozi wapya katika nafasi za Naibu mwenyekiti, pamoja na wenyeviti wa Kamati mbalimbali za Halmashauri ambapo Mh.Nestory Godfley Chirumba Diwani wa kata ya aliweza kuibuka kuwa mshindi,na Mh.Nestory Diwani kata ya makong'onda ameibuka mshindi na kuwa mwenyekiti wa kamati ya Maadili, na Mh.Mahelela Diwani kata ya Chikoropola nae amekuwa mshindi na kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, pamoja na Mh.Arafati Diwani kata ya Namalenga nae ameibuka na ushindi na kuwa mwenyekiti kwenye kamati ya Uchumi.
.Madiwani katika Taarifa zao wameelezea Ujenzi mbalimbali wa miundombinu unaoendelea katika Kata zao ikiwemo Ujenzi wa madarasa, nyumba za walimu, zahanati, vituo vya Afya, miundombinu ya maji, na vyoo. Aidha, wametoa pongezi za dhati kwa Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dr, John Pombe Magufuli kwa kupeleka fedha za miradi vijijini katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu, Afya, Maji pamoja na mawasiliano.
.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa