Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Masasi Beatrice Mwinuka anawatangazia Wananchi wote kuwa, kuanzia Tarehe 27/05/2024 hadi tarehe 31/05/2024 watakuwepo Madaktari bingwa na Madaktari wabobezi wa Magonjwa ya akina Mama na uzazi, Watoto, Upasuaji, Ganzi na usingizi, pamoja na Magonjwa ya ndani (Shinikizo la damu, kisukari n.k)
Huduma hizo za kibingwa ambazo zitatolewa kuanzia wiki ya Tarehe 27/05 - 31/05/2024 zitatolewa katika hospital ya Wilaya ya Masasi iliyopo Maeneo ya Mbuyuni kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
MADAKTARI BINGWA WA RAIS SAMIA, TUMEKUFIKIA, KARIBU TUKUHUDUMIE.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa