Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia imetoa kiasi cha fedha shilingi 1,416,866,066/= kwa ajili ya ujenzi mpya wa shule ya msingi LUKULEDI MAALUMU iliyopo katika kata ya Lukuledi, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ikiwa na lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji kwa kuhakikisha kuwa kundi hili la wanafunzi wenye mahitaji Maalumu wanapata Elimu bora na yenye tija kwao, kutokana na kiasi hicho cha fedha kilichotolewa serikali inajenga miundombinu mbalimbali kwenye shule hiyo huku ujenzi ukiendelea kushika kasi ikiwemo.
1.Jengo la utawala moja
2.Madarasa kumu na mbili pamoja na samani zake,
3.Mabweni manne pamoja na samani zake.
4.Bwalo la chakula na Jiko
5.Nyumba za watumishi nne
6.Nyumba ya Mkuu wa chuo
7.Tanuru la taka.
8.Vyoo matundu tisa
9.Resource room
10.Chumba cha upimaji
11.Karakana ya magari na upishi
12.Karakana ya umeme na useremala
13.Karakana ya ushonaji na saluni.
jengo la utwala shule ya msingi Lukuledi Maalumu likiwa katika hatua za mwisho
Moja kati ya madarasa kumi na mbili yanayoendelea kujengwa katika shule ya Msingi Lukuledi Maalumu yakiwa katika hatua za umaliziaji.
Hii ni nyumba ya Matroni katika shule mpya ya msingi lukuledi Maalumu ikiwa katika hatua za umaliziaji.
Moja kati ya mabweni ya wanafunzi wa shule ya Msingi Lukuledi Maalumu yakiwa yanaendelea na ujenzi wake yakiwa katika hatua za umaliziaji.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa