Licha ya kuwepo changamoto mbalimbali nchini ikwemo baadhi ya Wazazi/walezi kutojua umuhimu wa kuwapeleka Watoto Shule kujifunza, Serikali bado inaendelea kuwajengea uwezo wa elimu ya awali kwa walimu katika maeneo mbalimbali nchini ili waweze Kutoa elimu bora kwa Watoto.
Uamuzi huo umekuja baada ya kuzinduliwa ile programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali (PJT- MMMAM ambayo inataka kutekeleza afua tano za Afya, lishe, Elimu, malezi yenye mwitikio, na ulinzi pamoja na Usalama kwa Watoto.
Mwalimu Tatu Kazibure ni Afisa elimu vifaa na takwimu, ambaye pia ni mratibu wa miradi ya Boost kutoka Halmashauri ya Wilaya Masasi amesema kwamba, halmashauri inafanya mafunzo hayo kwa walimu wanaofundisha madarasa ya awali na walimu wakuu wapatao 120 kutoka kwenye shule 68 ambazo zimeteuliwa na wizara yanayohusiana na suala zima la ufundishaji katika madarasa ya awali.
Amesema " mafunzo haya ni ya kitaifa ambapo yanaendelea katika maeneo mengine nchini Tanzania na Mkoa wetu wa Mtwara Halmashauri ya Wilaya Masasi ni miongoni mwa halmashauri ambazo walimu wetu wa madarasa ya awali wanapata haya mafunzo, kwaiyo hapa tuna jumla ya walimu 120 wamehudhuria lakini walitakiwa wawe walimu 136 lakini walimu 16 wamekosekana kwasababu mbalimbali."
Ameongeza kuwa mafunzo hayo ambayo yameanza Leo tarehe 09/01/2025 katika ukumbi wa zamani wa Halmashauri hiyo uliopo Masasi mjini ni ya siku tatu kwa walimu wakuu na siku nne kwa walimu wa awali ambapo yamelenga hasa kwenye matumizi ya ya njia na na vifaa vilivyoboreshwa vya mtaala wa Elimu ya awali kupitia program ya boost.
" Kwaiyo katika mafunzo haya sasa sisi Kama Halmashauri tunatarajia kwamba walimu watajifunza mambo mbalimbali kuhusiana na mtaala wa elimu ya awali kupitia mwongozo wa MUVETA, mwongozo wa UWAWA, na mwongozo wa vituo shikizi, lakini haya yote yapo kwa ajili ya kuijenga elimu ya awali kwamba mtoto anaposoma kwenye elimu hii ya awali anatakiwa afanyiwe vipi, na lengo kubwa pia ni kuifanya hii elimu ya awali inamjenga mtoto Kujua kiakili, kimwili,na kimaono huku akiweza kufanya vitu mbalimbali kulingana na umri wake."
Aidha mwalimu Kazibure amehitimisha kwa kuwaomba walimu wote ambao wamefikiwa na mafunzo hayo kwamba wayatumie vizuri ikiwemo namna ya kuandaa maandalio ya somo, mada changamshi, maazimio ya kazi, utengenezaji wa zana mbalimbali ambazo zitakuwa zinasaidia katika suala zima la ujifunzaji na ufundishaji ambapo wanategemea kupata matokeo chanya na Kuleta mabadiliko katika madarasa ya awali.
09/01/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa