Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wametakiwa kuhakikisha wanavitunza vifaa vyote vitakavyotumika katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura na kuzingatia wanayafanyia kazi kwa usahihi maelekezo yote yatakayotolewa na Tume wakati zoezi hilo litakapokuwa limeanza.
Wito huo umetolewa leo tarehe 21/01/2025 na Afisa mwandikishaji Jimbo la Lulindi na Ndanda halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi.Hadija Mkumbwa wakati akifungua semina ya mafunzo ya uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wapatao 34 kutoka ngazi ya halmashauri.
Amesema semina hiyo ambayo ni ya siku mbili kuanzia tarehe 21-22 january 2025 imelenga kutoa elimu ya kutosha itakayowawezesha kutekeleza majukumu yao ili kufanikisha zoezi hilo ambapo pia yanahusisha namna bora ya ujazaji wa fomu, kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura, pamoja na matumizi sahihi ya vifaa vya uandikishaji wa wapiga kura.
``tunatarajia kuwa baada ya mafunzo haya, nyie mtapaswa kutoa mafunzomliyopata hapa kwa waendeshaji wa vifaa vya bayometrik na waandishi wasaidiziambao watahusika na uandikishaji wa wapiga kura vituoni,ni matumaini yangu kuwabaadhi yenu mmewahi kushiriki katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Tumeikiwemo hii ya uboreshaji wa Daftari hivyo natarajia mtafanya kazi kwa weledi ,bidii na moyo wa kujituma ili kufaniisha zoezi hili la kitaifa``…alisemaBi.Hadija mkubwa.
Ameongeza kuwa katika jambo lingine muhimu ambalo linalenga kuleta uwazi katika zoezi zima ni mawakala wa vyama vya siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikishia wapiga kura ambapo pia watatumika kuwatambua wapiga kura wa eneo husika na hawatakiwi kuingilia utekelezaji wa majukumu ya watendaji wote wa uboreshaji wakati wote wa uandikishaji wapiga kura vituoni.
Pichani ni wanasemina wakila kiapo mbele ya Mhe. Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Masasi Bw.Shaibu Mzanda.Kiapo hicho ni kwa ajili ya Kujiondoa uanachama au kutokuwa mwanachama wa Chama cha Siasa na Kiapo cha Kutunza Siri katika zoezi lote la Uboreshaji wa Daftari la Kudmu la Wapiga Kura
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa