Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imeendelea kumshukuru mhe.Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia fedha kiasi cha shilingi milioni 67,300,000.00 kwa ajili ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa vyumba 2 vya madarasa na matundu 6 ya Vyoo vya wanafunzi wa awali katika Shule ya msingi Chikukwe.
Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi wa mradi huo iliyosomwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chikukwe Eliomega Rosiaeli Akyoo mbele ya Kamati ya Siasa(CCM) mkoa ambayo ilifanya ziara hivi karibuni ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekekezwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya Masasi, amesema kwamba mnamo tarehe 18/06/2024 shule ya msingi Chikukwe ilipokea fedha kiasi cha shilingi 67,300,000.00 ikiwa shilingi milioni 66,300,000.00 kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu ya wanafunzi wa awali na kiasi cha shilingi milioni 1,000,000.00 kwa ajili ya Usimamizi wa miradi ngazi ya shule kupitia fedha za programu ya BOOST.
"Mradi huu ulitakiwa kutekelezwa ndani ya siku 90 ila kwakuwa wakati fedha hizi zinaingizwa ilikuwa ni kipindi cha mwisho wa mwaka wa Serikali hivyo fedha hizi zilianza kutumika Kama bakaa ya fedha za mwaka 2023/2024, kwenye bajeti ya mwaka 2024/2025 hivyo utekelezaji wa mradi huu ulianza tarehe 15/08/2024 na ulitakiwa kukamilika tarehe 15/11/2024 hivyo mpaka sasa kiasi cha shilingi 57,637,376.00 kimetumika na kiasi kilichobaki ni shilingi 8,662,624.00 na kinaendelea kutumika." alisema mwalimu Akyoo
Amesema mradi huo ambao unatekelezwa kwa njia ya force account, kwasasa mradi upo katika hatua ya umaliziaji, na kazi inayoendelea ni kufanya skimming na upakaji wa rangi.
Ameongeza kuwa katika utekelezaji wa mradi huo umepitia changamoto ya mfumo wa manunuzi wa NeST kwani zabuni mbalimbali za vifaa zilikuwa zinatangazwa na kurudiwa zaidi ya mara moja, Lakini upatikanaji wa wazabuni ulikuwa mgumu na ikizingatiwa muda wa utekelezaji wa mradi huo ulikuwa unapotea hivyo Halmashauri ililazimika kufanya manunuzi kwa njia ya Quatation ili kukamilisha mradi.
Ndg.Said Nyengedi ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Mtwara akizungumza Kwa niaba ya Kamati hiyo amesema kwa pamoja wanaishukuru serikali ya awamu ya sita ya chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kwasababu haikumuacha mtu yeyote na hii si hapo tu Chikukwe bali ni katika maeneo mengi maendeleo yanaonekana ili hata mtoto mdogo mzazi wake asipate shida yakuacha kwenda katika Shughuli zingine bali wawapeleke shule ili wapate elimu, na hilo ni jambo la kujivunia sana.
" Na hii niwaombe wazazi muwalete watoto shule, wakati mwingine tunasema watoto wa siku hizi mmomonyoko wa maadili, lakini kumbe mmomonyoko huu wa maadili unaanzia kwetu sisi wazazi, ukimpeleka mtoto maeneo haya atakuwa analelewa katika mazingira ya shule na atakuwa na nafasi ya kujifunza tabia njema , na hakuna kitu muhimu cha kumrithisha mtoto zaidi ya elimu ambayo itamsaidia katika maisha yake, niwaombe sana wananchi wa Chikukwe mliopo hapa muwe mabalozi kwa wananchi wengine msikubali watoto wenu wabaki majumbani bali waje wapate elimu hapa tena katika mazingira mazuri kabisa "..alisisitiza Nyengedi
Shule ya msingi Chikukwe ina jumla ya wanafunzi 747 ambapo wavulana ni 370 na wasichana 377.
10/01/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa