Halmashauri ya Wilaya Masasi Mkoani Mtwara imeibuka mshindi wa kwanza wa maonesho ya Nanenane kanda ya kusini kwa mwaka 2018 kati ya Halmashauri 15 za Mikoa ya lindi na Mtwara zilizoshiriki maonesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi baada ya kuwa banda bora kwa kuonesha tekinolojia kwa vitendo za Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
Wajasiliamali na watumishi wakishangili ushindi katika Maonesho ya Nanenane kanda ya Kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi tarehe 08.08.2018
Ushindi huo umetokana na banda hilo kuweza kutafsiri kwa vitendo kauli mbiu ya maonesho hayo ya “kuwekeza katika Kilimo mifugo na uvuvi kwa maendeleo ya viwanda” ambapo teknologia za kisasa zilioneshwa katika mashamba darasa ikiwemo faida za matumizi sahihi ya Pembejeo kama mbegu za kisasa na viwatilifu ili kuwa na uzalishaji wenye tija utakaopekelea viwanda kuwa na malighafi za kutosha.
Aidha Halmashauri ya Wilaya ya Masasi pia iliweza kuonesha kilimo jumuishi ambapo watu wenye ulemavu nao wanaweza kushiriki katika kujenga uchumi wa nchi kupitia shughui za kilimo cha busitani wakiwa nyumbani kwa kutumia vifaa rahisi kama makopo, mifuko mataili na vitu vingine ambapo wanaweza kuhudumia kwa urahisi bila kwenda mashamba ya mbali.
Kilimo cha Bustani ya Mbogamboga inayojumuisha makundi ya watu wenye mahitaji maalumu (walemavu)
Mbali na kuwa mshindi wa kwanza kwanza kati ya Halmashauri 15 za Mikoa ya Lindi na Mtwara katika maonesho hayo, Halmasauri ya Wilaya ya Masasi imekuwa mshindi wa pili wa jumla katika kilele cha maonesho hayo huku Jeshi la Kujenga Taifa likiibuka mshindi wa kwanza wa jumla.
Kutokana na ushindi huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe. Juma Satmah, amepongeza Idara ya kilimo, watumishi na wajasilimali wote walioshiriki katika maonesho hayo kwa mchango wao uliofanikisha ushindi huo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mhe. Juma Satmah akipokea kikombe cha ushindi (aliyevaa koti) kutoka kwa mgeni rasmi wa sherehe hizo Mhe Naibu Waziri wa TAMISEMI Joseph Kakunda (mwenye tisheti la kijani) katika kilele cha maonesho ya Nanenane kanda ya kusini yaliyofanyika katika viwanja vya Ngongo manispaa ya Lind. kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa
“Nawapongeza sana wote mlioshiriki katika maonesho haya hasa idara ya kilimo waliosimamia upandaji wa mazao kwenye mashamba haya ambayo yamefanya Halmashauri kuweza kuelezea uwekezaji wa kilimo, mifugo na uvuvi kisasa kwa vitendo kwa ajili ya kuzalisha malighafi za Viwanda na hatimaye kukuza uchumi” alisema Satmah
Bidhaa za wajasiliamali kwenye banda la Halmashauri ya Wilaya ya Masasi
Satmah ameeleza kuwa Halmashauri imeendelea kupata ushindi wa kishindo mara tano Mfululizo, hivyo inaonesha jinsi watumishi wanavyojituma na kujitoa katika kuwatumikia wananchi kwa kufanya mambo kwa weledi, “nawapongeza kwa hilo maana wanaijengea Heshima halmashauri yangu”
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Changwa Mkwazu alisema ushindi huo umetokana na kufanya kazi kwa ushirikiano lakini pamoja na kufanya kazi kwa kujituma sana hivyo ushindi huo unatupa deni la kujipanga zaidi katika maonesho yajayo ili kutetea ushindi huu tulioupata mara tano Mfululizo sasa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Changwa Mkwazu akipeana mkono wa Pongezi na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mhe Gelasius Byakanwa baada ya Halmashauri yake kupokea zawadi ya ushindi kwenye maonesho ya Nanenane 2018
Maonesho ya Nnanenane kwa mwaka 2018 yaliangazia katika kuongeza uzalishaji wa matumizi bora ya pembejeo na zana bora,uongezaji wa thamani ya Mazao kwa kufanya usindikaji na matumizi bora ya ardhi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa