• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kujua masuala ya Ardhi

KUJUA MASUALA  YA ARDHI

Nini maana ya ardhi

  • Ardhi ni sehemu ambayo ipo juu na chini ya uso wa nchi pamoja na mimea inayoota au kupandwa juu yake, majengo, mawe, milima n.k.
  • Ardhi hii inaweza kumilikiwa ba kundi la watu, mtu binafsi, taasisi na kusimamiwa na mamlaka mbalimbali.
  • Maji, madini na petroli sio sehemu ya ardhi chini ya sheria hii

Aina za ardhi:

  1. Ardhi ya kawaida (Ardhi ya Mijini)

Hii ni ardhi yote ya umma ambayo siyo ardhi ya hifadhi wala ya kijiji.

Ardhi hii inasimamiwa na Kamishna wa ardhi.

  1. Ardhi ya hifadhi  

Hii ni ardhi iliyohifadhiwa kama vile misitu ya hifadhi, mbuga za wanyama, vyanzo vya maji, barabara, ardhi yenye madhara n.k

Ardhi yenye madhara ni ile ambayo ikitumiwa bila tahadhari inaweza kusababisha uharibifu wa mazingira au kuhatarisha uhai.

Ardhi hi inasimamiwa na mamlaka za hifadhi au Afsa Mteule wa Serikali.

  1. Ardhi ya kijiji
  • Hii ni Ardhi ambayo mipaka yake imewekwa kwa sheria au utaratibu wa kiutawala kama ardhi ya kijiji kwa matumizi ya wanakijiji.
  • Ardhi hi inasimamiwa na Halmashauri ya kijiji.

Kubadili aina za ardhi (kuhawilisha):

  1. Inawezekana kubadili ardhi ya kawaida au ya hifadhi kuwa ardhi ya kijiji na kubadili ardhi ya kijiji kuwa ardhi ya kawaida au ardhi ya hifadhi.
  1. Ili kuweza kubadili aina za ardhi inabidi kufuata hatua zifuatazo:
  • Kama ni ardhi ya kawaida au ya hifadhi kuwa ardhi ya kijiji inabidi halmashauri ya kijiji kwa idhini ya mkutano wa kijiji itoe mapendekezo yao kwa Waziri kupitia Halmashauri ya Wilaya.
  • Kama ni Ardhi ya kijiji kuwa Ardhi ya Hifadhi au Ardhi ya kawaida inabidi mamlaka inayosimamia ardhi hiyo itoe mapendekezo yake kwa Waziri.
  • Waziri ataagiza tarifa itolewe kwenye gazeti la Serikali na kupelekwa kwa Halmashauri ya kijiji ikielezea mahali, ukubwa wa eneo na maelezo mafupi ya mapendekezo hayo.
  • Kama ni ardhi ya kijiji inabadilishwa kuwa ardhi ya kawaida au ya hifadhi inahitajika tarifa si  chini ya siku tisini (90).
  • Kama ni ardhi ya kawaida au ya hifadhi inabadidishwa kuwa ardhi ya kijiji inahitajika taarifa si chini ya siku sitini (60).
  • Kamishna au Afisa aliyeidhinishwa (k.m Afisa ardhi wa Wilaya) anatakiwa kuhudhuria mkutano wa Halmashauri ya kijiji au mkutano wa kijiji kufafanua sababu za mabadiliko na kujibu maswali yoyote.
  • Ardhi ya kijiji haitabadiliswa hadi pale tu malipo ya fidia yatakapokuwa yamekubalika.

ARDHI YA KIJIJI

Tafsiri ya ardhi ya kijiji

Ardhi ya kijiji ni kama ifuatavyo:

  • Ardhi iliyo ndani ya mipaka ya kijiji kiichosajiliwa (fungu 22 sheria ya serikali za mitaa)
  • Ardhi ilitengwa kama ardhi ya kijiji au mipaka yake imewekwa alama kama ardhi ya kijiji chini ya sheria yoyote au kwa taratibu za kiutawala kabla ya sheria hii kuanza kutumika.
  • Ardhi ambayo mipaka yake imetokana na makubaliano baina ya halmashauri ya kijiji husika na vijiji inavyopakana navyo, au wasimamizi wengine kama kamishna (Ardhi ya kawaida) na wasimamizi wa Ardhi ya Hifadhi.
  • Ardhi ambayo si ardhi ya hifadhi ambayo kwa muda wa miaka 12 kabla ya  tarehe 1 mei 2001 Sheria hii ilipoanza kutumika, wamilikaji wamekuwa wanaikalia na kuitumia kama ardhi ya kijiji.

Vijiji ndani ya Miji/Miji Midogo

  • Ardhi ya vijiji ndani ya miji midogo, itaendelea kuwa ardhi ya vijiji hadi hapo ardhi hiyo itakapotwaliwa kisheria na wanakijiji husika kulipwa fidia ipasavyo na kwa wakati.

Mipaka ya ardhi ya kijiji

Mipaka ya kijiji inatokana na:

  • Kubainishwa wakati wa kusajili kijiji.
  • Ilivyokwishawekewa alama chini ya sheria yoyote au taratibu za kiutawala.
  • Makubaliano baina ya Halmashauri ya kijiji husika na wasimamizi wenye mamlaka juu ardhi inayopakana na kijiji hicho kama vile:-

Halmashauri za vijiji jirani

Kamishna wa ardhi (Ardhi ya kawaida)

Wasimamizi wa hifadhi.

Mamlaka ya serikali ya mta au Mji.

Mtu au chombo anayekalia au kutumia ardhi kwa mujibu wa hakimiliki.

Utatuzi wa Migogoro ya Mipaka ya Vijiji

Halmashauri ya kijiji inapaswa kufanya kila juhudi kufikia makubaliano ya mpaka na majirani zake ikiwemo kuhusisha na kupata ushauri wa Halmashauri ya Wilaya husika.

Endapo juhudi hizi zitashindwa kufikia makubaliano au kutatua mgogoro, Sheria imeweka utaratibu kutatua migogoro ya mipaka ya Vijiji kama ifuatavyo:-

  • Waziri wa Ardhi atateua mtu kuwa msuluhishi kati ya kijiji na mtu au chombo ambacho kimeshindwa kuafikiana kuhusu mpaka, ili kusuluhisha na kushawishi kufikia makubaliano.
  • Kama msuluhishi atashindwa atamshauri Waziri kuteua mchunguzi ambaye atafanya uchunguzi kwa maelekezo na utartibu ulioainishwa katika hati ya uteuzi.
  • Wakati usuluhishi au uchunguzi unaendelea ni makosa kwa muhusika yeyote (Kijiji, mtu, chombo) kuchukua hatua zinazoweza kuathiri matokeo ya mgogoro.
  • Waziri atayakubali mapaendekezo yaliyotokana na uchunguzi kuwa utatuzi wa mgogoro wa mpaka labda kama ana sababu nzito zinazohusiana na maslahi ya umma.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • WAENDESHA VIFAA VYA BAYOMETRIKI NA WAANDIKISHAJI WASAIDIZI WAPATIWA MAFUNZO ILI KUFANIKISHA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA AWAMU YA PILI.

    May 15, 2025
  • WATAALAMU MASASI DC WAPATIWA MAFUNZO YA MATUMIZI YA MFUMO WA UJIBUJI HOJA ZA CAG.

    May 11, 2025
  • KAMATI YA FEDHA, UONGOZI NA MIPANGO YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO ROBO YA III (JAN -MACHI 2025) INAYOTEKELEZWA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI.

    May 06, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa