Halmashauri ya Wilaya ya Masasi ina jumla ya Shule za Msingi 135 zinazofanya Mtihani wa Upimaji kitaifa Darasa la nne 2025, huku shule mbili (02) zikiwa ni za watu binafsi.
Kwa upande wa Wanafunzi waliosajiliwa mwaka huu 2025 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi jumla ni wanafunzi 8,468 kati yao Wavulana ni 4, 319 na Wasichana 4,149 wakiwemo 96 wanafanya kwa lugha ya kiingereza ( English medium).
Hata hivyo katika taarifa yake aliyoitoa jana tarehe 21 Oktoba 2025 mbele ya Waandishi wa Habari jijini Dar Es Salaam,.Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani (NECTA) Profesa Said Ally Mohamed alisema upimaji kitaifa wa darasa la nne ni muhimu kwa kuwa huwezesha kufahamu viwango vya Wanafunzi katika kumudu stadi za juu za kusoma, kuandika na kuhesabu.
"Maandalizi yote yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambaza kwa karatasi za upimaji pamoja na nyaraka zote muhimu zinazohusu upimaji huo katika Halmashauri au Manispaa zote nchi nzima, wasimamizi wote wameshapewa semina na vituo vimekamilika vyote ".
Pia alisisitiza kamati zote za Mitihani ziweke mikakati ya kuzuia mianya yote itakayosababisha kutokea kwa udanganyifu na wasimamizi wote walioteuliwa wafanye kazi kwa umakini na kuzingatia uadilifu wa hali ya juu.
Hata hivyo ifahamike kuwa jumla ya Wanafunzi wote wa darasa la nne waliosajiliwa mwaka huu ni 15, 82140 wanafanya mtihani wa upimaji kitaifa kuanzia tarehe 22 - 23 Oktoba 2025 ambapo kati yao Wavulana 764,290 sawa na asilimia 48.31 huku wasichana wakiwa 817,850 sawa na asilimia 51.69.
Imeandaliwa na: Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini (H/W) Masasi
22/10/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa