Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi bibi Changwa M. Mkwazu aliyevaa (ushungi) akipata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa wizara ya kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu kabda ya kukabidhiwa hundi hizo leo tarehe 13.06.2017 ofisini kwake mbele ya watumishi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii na Mhasibu.
Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu Wizara ya Kazi, Ajira ,Vijana na Wenye Ulemavu imetoa mikopo kwa vikundi vinne vya vijana katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wenye thamani ya shilingi milioni 16,000,000.00 kwa ajili ya kuwawezesha vijana kiuchumi kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujasiliamali.
Akizungumza wakati wa kukabidhi hundi hizo Mkurugenzi Msaidizi wa Utaratibu Uwezeshaji wa Vijana Kiuchumi bibi Ester Riwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo bibi Changwa M Mkwazu, ofisni kwake alisema wizara hutoa mikopo kwa vikundi vya vijana ambavyo vinakuwa vimekidhi vigezo vya kukopeshwa ikiwemo andiko bora la mradi lengo ikiwa ni kuwasaidia kukuza uchumi kwa kujiajiri.
“Wizara inajitahidi kuhakikisha inatoa mikopo kwa vijana wanaoonesha nia ya kuanzisha miradi ya ujasiliamali kama njia ya kujiongezea kipato na kukuza miradi yao wakiwa kwenye vikundi, hivyo vijana wachangamukie fursa hii ya kujuinga kwenye vikundi ili waweze kukopesheka na hatimaye waweze kujikwamua kuichumi” alisema Riwa.
Akiongea baada ya kupokea hundi hizo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya masasi bibi Changwa M Mkwazu aliishukuru serikali kwa kutoa mikopo hiyo kwa vijana kwani Halmashauri pekee haiwezi kutoa mikopo kwa vikundi vyote maana ni vingi.
Aidha Mkwazu amesema Halmashauri itajitahidi kuhakikisha marejesho yanafanyika kwa wakati lakini pia kuhimiza vikundi vingine vya vijana kuandika maombi ya kuomba mkopo ikiwa ni pamoja na kuwasaidia namna bora ya kuandika maandiko hayo.
Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi jumla ya vikundi 9 vilituma maombi ya kuomba mkopo lakini ni vikundi vinne Vikundi ndivyo vilivyopata mkopo huo ni kikundi cha kikundi cha Mshikamano, Jikwamue, Chimutu na Napata.
Halmashauri imeendelea kutenga 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya kuwezesha Mfuko wa wanawake na vijana ili kukuza mitaji kwa vikundi vya wajasiriamali vya wanawake na vijana ambapo kwa mwaka 2015/2016 Jumla ya Tsh. 160,770,000 kwa vikundi 95 zimekopeshwa na kwa mwaka 2016/2017 Tsh. 225,500,000 zimekopeshwa kwa vikundi 75.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa