Waziri wa Kilimo Hussein Bashe ametoa saa 24 kwa kampuni ya RV inayonunua mazao Masasi mkoani Mtwara kulipa madeni ya wakulima huku akiagiza vyombo vya ulinzi na usalama Wilayani humo kuwashikilia viongozi wastaafu wa ushirika ambao wamehusika na ubadhirifu wa zaidi ya shilingi Milioni 139.
Waziri Bashe ametoa maagizo hayo wakati alipohutubia Wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Chiwale Halmashauri ya wilayani Masasi mkoani Mtwara ambapo alifahamishwa kuwa baadhi ya wakulima wa korosho ambao ni wanachama wa Chama cha Msingi cha Ushirika cha Nanyindwa AMCOS hawakulipwa kiasi cha TZS milioni 139 katika msimu wa 2016/17 hatua iliyosababisha mali za AMCOS hiyo ikiwemo trekta na lori kupigwa mnada kwa amri ya mahakama.
Pia amesema serikali inakwenda kufumua mfumo wa mauzo na ugawaji wa ruzuku za pembejeo kwa kuwa hauna uwazi.
Akizungumza katika mwendelezo wa ziara yake katika mikoa ya Kusini, Waziri Bashe ameelekeza kampuni ya RV ambayo ilishiriki mnada wa mbaazi kuhakikisha inalipa wakulima pesa ndani ya saa 24.
Amesema "katibu wa Chama cha Msingi na hawa watu 15 watafutwe,lakini kama Kweli wapo mitaani wanatembea na wengine ni waheshimiwa Madiwani, mimi ninadhani watu wa vyombo vya Ulinzi na usalama milioni 139 na na waliohusika wanajulikana,sasa matokeo yake hicho Chama cha Msingi trekta lao limeuzwa,mali zao zimeuzwa na waliofanya uhalifu wapo mitaani wanatembea, TAKUKURU yupo ana Mamlaka yakuwashughulikia hawa wanaohujumu uchumi, chukueni hatua dhidi ya hawa watu waliofanya ubadhirifu, wizi ambao umesababisha hasara ".
Aidha mhe.Bashe ameongeza kuwa haiwezekeni katika Chama cha Msingi malipo yamefanyika Kwa mkulima alafu wapo Wakulima wengine wamelipwa ziada haiwezekeni, haiwezekeni Chama cha Msingi kilipe malipo ya ziada kwa mkulima kwaiyo vyombo vitusaidie kuchunguza vichukue ile risiti ya Wakulima ninani amesaini fomu ya malipo anza kukamata huyo, wale waliolipwa ziada watafutwe na warudishe fedha zote ili wakulima ambao hawajapata haki yao wapatiwe, chukueni hatua haina maana 4R za mheshimiwa Rais haihalalishi haya mambo ".. alisisitiza mhe.Bashe
Viongozi wanaolalamikiwa ni pamoja Diwani wa Kata hiyo ya Chiwale Yusuph Mataula aliyekuwa Katibu wa Amcos ambaye anatuhumiwa kutokana na tuhuma mbalimbali za ubadhirifu wa fedha za Wakulima na Hashim Pahala aliyekuwa Mtendaji wa kijiji ambaye anatuhumiwa kuuza shamba hewa kwa mkulima.
02/10/2024
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa