Kutokana na kanda ya kusini yaani Mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma kukithiri kwa vitendo vya uchomaji moto kwenye misitu iliyohifadhiwa na ya kawaida, Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Kanda ya Kusini imekuja na mfumo mpya wa kutambua na kufuatilia kwa haraka uwepo wa moto kwenye misitu kwa kutumia njia ya matandao na kutoa taarifa za kuuzima mapema kabla haujasababisha madhara makubwa kwenye msitu.
Washiriki wakifuatilia hatua mbalimbali za kuzingatia juu ya matumizi ya mfumo mpya wa utambuaji na udhibiti wa moto kwenye misitu
Kutumia mfumo huo wa kimtandao, wataalamu wa misitu watanweza kutambua uwepo wa moto haraka kwa kutumia mtandao badala ya kwenda kwenye eneo linaloungua hali ambayo ilikuwa inachelewesha utoaji wa taarifa lakini pia moto kusababisha eneo kubwa la msitu kuteketea kwa moto.
Mfumo huo mpya wa kukabiliana na mioto katika maeneeo mbalimbali ya misitu, umeelezwa leo na Mratibu wa Ufuatiliaji moto kwa njia ya satellite ndugu Kekilia Kabalimu kwa baadhi ya wataalamu wa misitu Kanda ya Kusini lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo wa namna ya kutumia njia ya mtandao kutambua na kufuatilia mioto inayotokea na hatimaye kuweza kuizima mapema kabla haijaleta madhara makubwa.
Kekilia ameeleza kuwa utambuzi na ufuatiliaji wa moto kwa njia ya mtandao itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uharibifu wa misitu kwa urahisi ambapo wataalamu wa misitu wataweza kutuma taarifa ya tahadhari ya mpema juu ya uwepo wa moto, hali ambayo itawasaidia kujiweka tayari kuudhibiti kwa hraka zaidi
Kekilia amewataka wataalam hao wa misitu kutoa taarifa kwa wananchi au jamii inayozungunga msitu juu ya uwepo wa moto kwenye msitu ili washiriki kuuzima moto huo kabla haujaleta madadha makubwa, vilevile watawajibika kuwaelimisha wananchi muda gani wanaweza kuchoma moto kwa kuzingatia uelekeo wa upepo.
Aidha Kekilia amesema kuwa kwa mwananchi ambaye anataka kuchoma moto wakati akisafisa shamba na kazi zingine azingatie ueleleo wa upepo kwakutumia njia ya kuweka kidole mdomoni na kukitoa na kuacha kikauke kwa dakika moja , upande utakaokauka haraka ndiko upepo unakotokea hivyo itampasa achome moto kwa kuangalia upande wa kidole ambao haujakauka kwani upepo unaongeza kasi ya moto kusambaa kwa haraka.
Akifungua mafunzo hayo mwakilishi wa Meneja wa Wakala wa Misitu Tanzania Kanda ya Kusini Mpokigwa Kibona amewasihi washiriki ambao ni wataalamu wa misitu kuwa makini katika mafunzo hayo ili wakaweze kupata uelewa mzuri wa namna ya kutambua , kufuatilia na kudhibiti mioto inayochomwa sana kwenye misitu ya hifadhi ikizigatiwa kanda ya kusini inashika nafasi ya tatu katika vitendo vya uchomaji moto misitu ovyo.
“Nitashangaa kama mtaalamu wa misitu uliyepata mafunzo haya lakini ukashindwa namna ya kutambua na kudhibiti moto kwa haraka na hatimaye kupelekea moto kusababbisha madhara makubwa ya kuharibu misitu sitakuelewa” alisema kibona
Mpokigwa Kibona akifungua mafunzo ya matumizi ya mtandao kutambua na kudhibiti moto kwa niaba ya Meneja wa Misitu kanda ya kusini leo katika ukumbi wa jengo la makao makuu ya Wakala wa Misitu Tanzania kanda ya Kusini
Atupokigwe ameeleza kuwa moto unaweza kutoea wakati wa kusafisha mashamba, vipisi vya sigara lakini pia uchomaji moto kwa makusudi, hivyo wataalamu wa misitu wanawajibu wa kuendelea kutoa elimu kwa jamii paoja na kutumia mfumo huo kutambua uwepo wa moto ili waweze kuudhibiti kwa haraka.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa