Ili kufika lengo la serikali la kupunguza maambukizi ya ugonjwa wa Ukimwi nchini ifikapo mwaka 2020, nguvu na jitihada zaidi zinahitajika katika kuzuia maambukizi mapya ya UKIMWI kwa kuboresha namna ya utoaji huduma katika ngazi ya jamii ikiwemo kuelimisha wananchi kupima afya zao ili kutambua hali zao huku wanaokutwa na maambukizi kuanza kutumia dawa na wasio na maambukizi kuendelea kujikinga.
Hayo yamebainishwa leo katika kikao cha wadau wa maendeleo wakiwemo wamiliki wa asasi mbalimbali za kiraia, taasisi za benki na taasisi za dini katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kilicholenga kujadili namna ya kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ambapo suala la kutoa elimu kwa jamii juu ya umuhimu wa kupima afya zao pamoja na kutumia dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi limejadiliwa ili kufikia lengo la kuwa na jamii isiyona maambuki ifikapo 2030.
Akizungumza katika kikao hicho, Afisa Mradi -programu ya uwezeshaji kamati shirikishi za waishio na virusi vya ukimwi na uboreshaji wa mifumo ya serikali za mitaa kupitia shirika la JSI ndugu Pamela Msei amesema kuwa, ili utoaji wa elimu ya kuhusu ukimwi iwafikie wananchi kamati za ukimwi ngazi ya jamii lazima zitumike kwani kupitia kamati hizo wananchi wengi wanaweza kupata elimu ya upimaji, matumizi ya dawa, kutonyanyapaa waathirika, elimu ya lishe na shughuli za uchumi.
“Tunaziwezesha kamati kuanzia ngazi ya kijiji hadi halmashauri ili kuwezesha mfumo bora wa utoaji wataarifa za masuala mbalimbali ya UKIMWI ikiwemo kujua idadi ya wagonjwa, mahitaji yao, pamoja na kuwafuatilia matumizi ya sahihi ya dawa” alisema Pamela.
Pamera ameeleza kuwa , Kila mdau wa maendeleo anayo nafasi ya kuchangia juhudi za serikali katika kuhakikisha maambukizi ya ukimwi Tanzania yanapungua ifikapo mwaka 2020 ambapo 90% ya watanzania wawe wamepima VVU, 90% waliokutwa na maambukizi wanatumia dawa na 90% walioanza kutumia dawa wanaendelea utumia na ifikapo mwaka 2030 maambukizi mapya iwe 0%, vifo vitokanavyo na UKIMWI 0% na unyanyanyapaa 0%.
Wakati juhudi za kutokomeza maambukizi mapya yakiwa yanaendelea, pia shughuli za uchumi zinapaswa kuendela hivyo watu wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI waliojiunga kwenye vikundi wanafursa ya kupata mikopo kama watu wengine.
Kwa upande wake mwakilishi wa Taasisi za dini shekhe Baina ameeleza kuwa pamoja na kuwa dini inasisitiza masuala ya kiroho, lakini pia inawasisitiza waumini kuwa n afya njema hivyo kila mtu ana wajibu wakupia afya lakini pia watu wawe waaminifu kwenye mahusiano lakini kama hujaoa achana na uzinzi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa