Waratibu elimu kata na wasimamizi wa vituo vya afya wakiwa kwenye mafunzo.
Serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na mradi wa uimarishaji mifumo ya sekta za Umma ujulikanao kwa Kiingereza kama Public Sector Systems Strengthening, (PS3) unaofadhiliwa na shirika la mandeleo ya kimataifa la marekani (USAID) imetoa mafunzo ya Mfumo wa Uhasibu na Utoaji Taarifa za Fedha kwa ngazi ya Kituo cha Kutolea Huduma [Facility Financial Accounting and Reporting System (FFARS)] kwa waratibu elimu kata na wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya lengo ikiwa ni kuwajengea uwezo juu ya upatikanaji wa taarifa sahihi katika mahesabu ya mapato na matumizi katika vituo vyao.
Hayo yamesemwa na Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi ndugu Mwajabu Mkindi wakati akifungua mafunzo hayo kwa niaba ya mkurugenzi wa halmashauri hiyo kwa waratibu elimu elimu kata na wasimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya kutoka halmashauri ya wilaya nay a mji masasi leo na kueleza kuwa kuundwa kwa mfumo huu kutasaidia kuhakikisha fedha za ruzuku zinasimamiwa vizuri, na taarifa za matumizi yake zinatolewa kwa usahihi, tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
Mkindi alisema kuwa mfumo huu kuhakikisha kwamba vituo vyetu vya kutolea huduma vinakuwa na mfumo maalum wa kuaandaa taarifa za mapato na matumizi, na hii itachangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, hususani kutimia kwa lengo linalotarajiwa kupitia fedha hizo.
Vilevile, Mkindi alieleza kuwa mfumo huo utafanya vituo vya kutolea huduma katika halmashauri zote mbili vinakuwa na mfumo maalum wa kuaandaa taarifa za mapato na matumizi, na hii itachangia uwajibikaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi, hususani kutimia kwa lengo linalotarajiwa kupitia fedha hizo.
Mkindi alikiri kuwa, kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa taarifa sahihi za rasilimali fedha zilizopo katika vituo vya kutolea huduma, hali inayopelekea halmashauri kushindwa kutoa taarifa sahihi za matumizi ya ruzuku zinazotolewa katika vituo hivyo, na wakati mwingine kusababisha halmashauri kupata hati ya mashaka kutoka kwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwani hakukuwa na mfumo sahihi wa kusaidia kuepukana na tatizo hilo.
Kutokana na uwepo wa mfumo huu mpya sasa, utasaidia kuhakikisha kunakuwa na muundo maalum wa kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi, na hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji wa vituo vya kutolea huduma kwa kutoa taarifa sahihi ya mapato na matumizi na hivyo kutoa fursa wananchi kuhoji pale atakapoona kuwa huduma zinazotarajiwa kupatikana katika vituo hazitolewi kulingana na ruzuku iliyotolewa.
Kwa upande wake msimamizi wa mafunzo hayo ndugu Elineema Kisanga ambaye ni mtaalamu wa masuala ya fedha alisema kuwa mafunza haya yanalenga kuboresha Nyanja tano ikiwemo masuala ya fedha, utawala bora na ushirikishwaji wa raia, rasilimali watu na tafiti tendaji ambapo mambo haya yote kwa pamoja yanatarahissha utendaji kazi katika taasisi za umma.
Kisanga alifafanua kuwa mafunzo hayo yameanza ngazi ya mkoa na sasa tupo ngazi ya Halmashauri ambapo wanaopata mafunzo haya leo watakuwa wawezeshaji kwenye maeneo yao ya kazi, hivyo nawaomba wanasemina wawe wasikivu ili waelewe vizuri na hatimaye wakawafundishe watumishi wenzao kwenye vituo vyao vya kazi.
Kisanga Mradi huu kwa sasa unatekelezwa katika mikoa 13 kwenye Halmashauri 95 hivyo tunategemea mabadiliko makubwa katika utoaji wa taarifa za mapato na matumizi kwenye vituo vya kutolea huduma za elimu na afya kwa sasa.

Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa