HALMASHAURI ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara imepata hati safi kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020 baada ya kufanya vizuri katika maeneo tofauti ikiwemo matumizi na ukusanyaj wa fedha, usimamizi wa mapato pamoja na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Brig Jen. Marco E. Gaguti ameipongeza Halmashauri ya wilaya ya Masasi, kwa kupata hati safi katika ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Brig Jen, Gaguti ametoa pongezi hizo Juni 17,2021 katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichoketi kwa ajili ya kujadili hoja za ukaguzi (CAG) kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri uliopo Mbuyuni na kuongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,Mh. Ibrahimu Chiputula.
Brig Jen, Marco Gagut amesema madiwani na watendaji kwa ujumla wanapaswa kuongeza nguvu zaidi katika ukusanyaji wa mapato na usimamizi bora wamatumizi ya fedha ili kuwa na ufanisi mzuri katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Ameliambia baraza hilo kuwa katika kipindi cha uongozi wake kama Mkuu wa Mkoa wa Mtwara atahakikisha kuwa fedha za serikali za miradi ya maendeleo zinatumika kama inavyokusudiwa na miradi yote ya maendeleo inakamilika kwa wakati na kwa ufanisi.
Katika hatua nyingine, Brig. Jen, Gaguti amewataka waheshimiwa madiwani, watendaji wa serikali na wananchi kwa ujumla Mkoani Mtwara kila mmoja kwa nafasi yake kuweka mkazo wa kuhubiri na kuimarisha suala la ulinzi na usalama ndani ya Mkoa wa Mtwara ili amani iliyopo hivi sasa iyendelee kuwepo.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri, Mhe. Ibrahimu Chiputula amesema Halmashauri itaendelea kusimamia kikamilifu matumizi ya fedha za miradi ya maendeleo ili Halmashauri hiyo iendelee kupata hati safi ya ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa kipindi kijacho.
Kwa upande wa wajumbe ambao ni waheshimiwa madiwani wamesema kuwa watahakikisha wanaonyesha ushirikiano wa pamoja na mkuu wa Mkoa kwa mambo mbalimbali ya kiuchumi na Maendeeleo ili kuhakikisha mapato ya Halmashauri yanaongezeka.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa