Katika Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Mwenge wa uhuru mwaka 2019 wenye Kauli Mbiu "Maji ni Haki ya Kila Mtu,Tutunze Vyanzo Vyake na Tukumbuke Kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa" umeweka Mawe ya Msingi katika Miradi miwili yenye Thamani ya shilingi 5,541,953,429.12/= na Kufungua Mradi mmoja wenye Thamani ya shilingi 55,920,000/= pia Umegawa hundi za Mikopo kwa wajasiriamali zenye Thamani ya shilingi 38,000,000/= kwa vikundi 19(Vijana 3, Wanawake 12, na Watu wenye ulemavu 4. Mwenge pia umegawa kadi za Bima ya Afya zenye Thamani ya shilingi 1,190,000/=,Umeona na kukagua mradi wa utunzaji wa vyanzo vya maji vinavyotunzwa kwa thamani ya shilingi 52,755,994.12/= kwa mwaka. umeona pia na kukagua banda la maonyesho ya Maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2019 na kuzindua klabu ya wapinga Rushwa moja. Jumla ya miradi yote ni shilingi 5,541,953,429.12/= kati ya fedha hizo shilingi 37,125,240/= sawa na asilimia 0.6 ni Elimu ya kujitegemea, shilingi 20,510,000/= ni mchango wa jamii sawa na asilimia 0.4, shilingi 55,288,800/= sawa na asilimia 1.0 ni Mchango wa Halmashauri, shilingi 5,376,273,395/= sawa na asilimia 97.0 ni fedha kutoka serikali kuu na Taasisi binafsi shilingi 52,755,994.12/= sawa na asilimia 1.0.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali ameweka Jiwe la Msingi katika Madarasa Mawili na chumba kimoja cha ofisi ya Walimu katika Shule ya Msingi Chikundi iliyopo kata ya Chikundi , ambayo kukamilika kwake kutawapunguzia wanafunzi wa Kata hiyo mrundikano wa wanafunzi wengi kwenye chumba kimoja cha Darasa ambapo mradi huu umegharimu kiasi cha shilingi
Shule ya Msingi Chikundi ipo katika kijiji cha Chikundi Kata ya Chikundi. Shule hii ni miongoni mwa Shule nne (4) za Msingi zilizopo katika Kata hii. Shule ina jumla ya wanafunzi 880, wakiwemo wavulana 428 na wasichana 452 Shule ina Walimu 16 wakiwemo walimu wa kiume 5 na walimu wa kike 11.
Hali ya miundo mbinu ya shule a msingi Chikundi
AINA
|
MAHITAJI
|
YALIYOPO
|
UPUNGUFU
|
Madarasa
|
24
|
14
|
10
|
Vyoo
|
39
|
18
|
21
|
Mwezi Januari mwaka 2019 uongozi wa shule ya msingi Chikundi ulipokea fedha kiasi cha Shilingi 46,600,000/= kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na matundu sita ya vyoo. Chanzo cha fedha hizi ni mradi wa EP4R kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Kwa kuzingatia uhaba wa vyumba vya ofisi za walimu na vyoo vya walimu uongozi wa shule uliongeza ujenzi wa chumba cha ofisi katika madarasa yanayojengwa na matundu mawili ya vyoo vya walimu.
Ujenzi wa vyumba hivi wiwili vya madarasa kupitia fedha za mradi wa EP4R ulianza mwezi April na kukamilika mwezi Julai 2019. Kuchelewa kuanza kwa mradi kulitokana na kuchelewa kuingiiziwa vifungu vya malipo katika mfumo wa fedha unaotumika na shule (FARRS) kutoka TAMISEMI.,
Katika ujenzi wa vyumba hivi vya madarasa na matundu ya Vyoo, wananchi wameunga mkono jitihada za serikali yetu kwa kujitolea nguvu zao katika shughuli mbalimbali ikiwemo Kuandaa eneo la ujenzi, kuchimba Msingi, kujaza kifusi, kumwaga jamvi na kuchimba shimo kwa ajili ya ujenzi wa matundu 6 ya vyoo. Kitendo hiki kiliiwezesha Shule kufanikisha ujenzi huu ukamilike kwa haraka na pia pesa iliyobakia ilisaidia kuongezea chumba cha ofisi na choo cha walimu matundu mawili ambacho kipo katika hatua ya ukamilishaji.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2019, Ndg. Mzee Mkongea Ali akikabizi Hundi za mikopo kwa wajasiliamali mbalimbali wa Halmashauri ya wilaya masasi zenye thamani ya shilingi 38,000,000/= wakiwemo wanawake,walemavu na wanaume vikundi hivyo vilivyonufaika ni pamoja na Maisha mapya sh.3,000,000/=,Tusaidiane sh.1,000,000/=, Mtujali sh.1,000,000/=, Umoja sh.1,000,000/=, Umoja vvu sh. 3,000,000/=, Mwendokasi sh.1,000,000/=, Tathmini sh. 1,000,000/=, Msimamo sh. 4,000,000/=, Mwamko sh.1,000,000/=, Mapambano sh.2,000,000/=, Tupendane Vikoba sh.3,500,000/=, Tumaini kata ya Mitesa sh.2,000,000/=, Mwamko kata ya Chikundi sh.1,000,000/=, Jipe Moyo kata ya Mpeta sh.1,000,000/=, Tuinuane kata ya Chikundi sh.2,000,000/=, Upendo kata ya Mwena sh.1,000,000/=, Tushikamane kata ya Ndanda sh.2,000,000/=, Mshikamano Namba 4 kata ya Chiungutwa sh.3,500,000/= na Amkeni Vijana kata ya Namalenga sh.3,000,000/=
Ujenzi wa Mradi huu wa maji wa Mwena – Liloya, ambao upo katika Kata nne za Mwena, Chikundi, Chigugu na Chikukwe ulianza kujengwa rasmi katika mwaka wa fedha wa 2017/2018, hii ikiwa ni utekelezaji wa nia ya Serikali ya kuwapatia wananchi hususani wananchi wa vijijini Maji safi na salama. Mradi huu unajengwa kwa kutumia chanzo cha maji ya chem chemi cha Mwena kilichopo katika Kijiji cha Mwena. Mradi huu utakapokamilika, utahudumia jumla ya vijiji 18 vya Mwena, Chibwini, Ndunda, Msigalila, Namali, Chikundi, Mkalapa, Mbaju, Chigugu, Mbemba, Mkuyuni, Mandiwa, Chikukwe, Maparagwe, Liloya, Mwambao, Mtunungu na Mji mwema vyenye jumla ya wakaazi wapatao 40,800. Hii itaongeza hali ya upatikanaji wa maji katika Halamashauri ya Wilaya ya Masasi toka asilimia 64 ya sasa na kufikia zaidi ya asilimia 80 ya wakazi wote.
Mradi huu unajengwa na Mkandarasi STC CONSTRUCTION COMPANY LIMITED kwa gharama ya shilingi 5,329,673,395/= ambapo awamu ya kwanza ilikuwa ni Mkataba wa Tsh. 4,471,710,595.00/= na mkataba wa Tsh.857,962,800.00 kwa awamu ya pili. Pia wananchi wamejitolea maeneo yao yenye thamani ya Tsh. 10,000,000/=kwa ajili ya kupisha ujenzi wa mradi huu. Mpaka sasa Mkandarasi ameshalipwa Tsh 3,551,150,776.36 sawa na asilimia 66.63 ya fedha yote. Mradi huu ulitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Septemba, 2019 ambapo hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 85.
Kukamilika kwa mradi huu kutawapunguzia kinamama adha ya kufuata maji mbali na maeneo yao na hivyo kuwapa nafasi kushiriki katika kazi nyingine za maendeleo ya kukuza uchumi wa Taifa na familia zao. Kwani kabla ya mradi huu wananchi hasa kinamama walitumia muda mwingi kutafuta maji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.
Shule ya Sekondari Ndanda ni moja kati ya Shule 4 za Halmashauri ya Wilaya ya Masasi zenye kidato cha tano na sita yenye Wanafunzi wavuana 908. Shule hii ina jumla ya watumishi 40, kati ya hao walimu ni 29 na wasiokuwa walimu ni 11. Aidha shule hii ilipata usajili rasmi mwaka 1928 ikiwa inamilikiwa na Shirika la Dini na baadaye kuchukuliwa na Serikali mwaka 1966.
Shule ya Sekondari Ndanda ina mahitaji ya nyumba za Watumishi 40 na zilizopo kwa sasa ni 30 na upungufu uliyopo ni 10. Kulingana na changamoto ya upungufu wa nyumba za watumishi, uongozi wa Shule walianza kukarabati nyumba 4 za Watumishi wa Shule. Kwa kutumia mfuko wa Elimu ya Kujitegemea unaojumuisha miradi kama vile duka, kilimo, ufugaji wa kuku wa nyama na mayai, stationery na saluni ya kiume. Baada ya kukamilisha kazi ya ukarabati huo ikaonekana sasa ni vema kuanza kujenga nyumba ya walimu (two in one) kwa kutumia mfuko huo wa Elimu ya Kujitegemea (EK).
Kazi ya ujenzi wa nyumba ya walimu umefanyika kwa mtindo wa kujitolea kupitia siku maalumu iliyoanzishwa na Shule ijulikanayo kama siku ya UZALENDO (UZALENDO DAY) ambapo siku hii wanajumuiya wote wa Shule ya Sekondari Ndanda kuanzia Mkuu wa Shule, walimu, watumishi wasio walimu na wanafunzi hujitolea kufanya shughuli mbalimbali Kupitia siku hiyo. Kazi zinazofanyika ni pamoja na kufyatua tofali hivyo Shule ilifanikiwa kuwa na benki ya matofali ambayo yametuika katika ujenzi wa nyumba hii.
Pia Viongozi wa Wilaya na Mkoa waliunga mkono jitihada za shule za kutengeneza matofali kwa kujitolea nguvu zao kuandaa eneo la ujenzi, kuchimba msingi, na kujaza kifusi. Kitendo hicho kiliwezesha shule kufanikisha ujenzi huu kwa haraka na kwa gharama nafuu na kuokoa fedha ambazo zimepelekea ujenzi kufikia mwonekano huu
Ujenzi wa nyumba ya walimu hadi sasa umegarimu Shilingi 54,414,040/= umefanyika kwa awamu mbili kama ifuatavyo:-
Awamu ya kwanza, Katika awamu hii ilijumuisha shughuli za kuandaa eneo, kuchimba msingi, kujenga Msingi na Boma. Inakadiliwa kiasi cha Shilingi 28,822,500/= zilitumika kwenye awamu hii
Awamu ya pili ilijumuisha shughuli za upauaji na umaliziaji wa nyumba, katika umaliziaji, shughuli zilizofanyika ni kupiga plasta,kuweka milango na madirisha. Jumla ya shilingi 25,591,540/= zilitumika. Chanzo cha fedha hii ni shilingi 17,288,800/=zimetoka Halmashauri ya Wilaya ya Masasi kutoka mfuko wa Elimu na kiasi cha Shilingi 8,302,740/= ni za Elimu ya Kujitegemea (EK) kutoka Ndanda Sekondari
Ujenzi huu utasaidia kupunguza tatizo la upungufu wa nyumba za Watumishi wa Shule kutoka upungufu wa nyumba 10 hadi kufikia upungufu wa nyumba 8. Pia hali hii itapunguza adha ya walimu waliolazimika kupanga mbali na shule tena kwenye mazingira magumu na kusababisha kushindwa kufanya maandalizi ya shughuli za kufundishia na kujifunzia.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa