Wananfunzi wa shule kutoka katika Wilaya za Masasi na Nanyumbu wamehimizwa kushiriki michezo kikamilifu kutokanana na michezo kuwa njia nzuri kwa wananfunzi hao kuwa na afya njema ya akili na mwili hali ambayo itawasaidia kutimiza ndoto zao za kielimu na kuendeleza vipaji vyao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halamashauri ya Wilaya ya Masasi bibi Changwa M Mkwazu wakati wa uzinduzi wa mashindano ya michezo ya UMITASHUMTA kanda ya Masasi yanayofanyika katika shule ya sekondari Abbey Ndanda kuanzia jana tarehe 8.06.2017 ambapo wanafunzi kutoka wilaya ya Masasi na Nanyumbu wanashiriki katika michezo ya aina mbalimbali.
Bibi Changwa aliwaeleza wanamichezo hao kuwa michezo ina faida kubwa katika maisha yenu kiafya ambapo kupitisha michezo mtaepuka kupata mgonjwa yanayotokana na kutofanya mazoezi kama vile shinikizo la damu, kuwa na uzito mkubwa zaidi na mengine ambayo yatasababisha mshindwe kutimiza ndoto zenu za kielimu lakini pia kusababisha kifo.
“Suala la michezo ni mhimu kwa ustawi wa afya zetu na uchumi kwani jamii yenye watu ambao hawana afya njema itakuwa masikini kwani hataweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za uchumi hali ambayo itapelekea kuwa na watu masikini, kutokana na hali hiyo ndio maana serikali imefanya kila jumamosi ya pili kila mwezi kuwa siku ya mazoezi nchi nzima” alifafanua Changwa.
Changwa aliongeza kuwa pamoja na kuwa michezo kuwa ni afya lakini pia ni chanzo cha ajira kwani wenye vipaji vya mchezo Fulani watapata fursa ya kuchaguliwa kuwa wachezaji wa timu mbalimbali za ndani na nje kama baadhi ya watanzania wenzetu ambao wanachezea timu za taifa, vilabu mbalimbali na wanapata kipato kikunbwa kama vile Mbwana Samatta (Mtanzania),Ronaldo wa Ureno, Messi wa Algentina na wengine wengi.
Bibi Changwa alitoa rai kwa wanamichezo wote kuwa na nidhamu katika michezo, alisema “ mmetoka kwa wazazi wenu mkiwa salama, msituangushe, msije mkawa vijana wabaya mkapata maradhi lakini pia mjiepushe utumiaji wa lugha chafu na matusi, uvaaji mbaya mkazitia aibu wilaya zenu”.
Aliwaomba Maafisa Michezo na walimu walezi wa watoto hao kuhakikisha watoto wanatunzwa vizuri ili kufanya lengo lao linafikiwa na kurudi salama kwa wazazi wao ili kujenga imani kwa wazazi , waepuke kabisa na mambo ambayo yatawatoa nje ya lengo la michezo, alisema “ nina maana kwamba watoto walelewe kwa kujali jinsia zao kama ambavyo tunalea watoto wetu na baada ya michezo hii kuisha hatutapenda kusikia kesi zozote za utovu wa nidhamu na maadili”.
Alitumia fursa hiyo kuwashukuru waliotoa ufadhili wa hali na mali ambo ni mkuu wa shule ya sekondari ya Abbey kwa kuruhusu kutumia eneo lake kwa mashindano, pia mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ndanda na Njenga kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo malazi kwa siku zote za mashindano.
Akisoma risala mbele ya mgeni rasmi mratibu wa mashindano hayo kwa upande wa Halmashauri ya wilaya ya masasi Mwalimu Fadhili Swalehe (Shule ya msingi Mkalapa) alisema mashindano haya yalianza toka ngazi ya shule, kata na sasa kanda na kisha yatafanyika katika ngazi ya mkoa ambapo baada ya kupata wachezaji bora watakwenda kushindana ngazi ya Taifa.
Mwalimu Swalehe alisema katika ngazi hii ya kanda kuna jumla ya wanafunzi 180 na walimu 27 kutoka halmashauri tatu(masasi, Nanyumbu na Masasi Mji) na baada ya mashindano hayo wanategemea wanamichezo 100, walimu wa michezo na viongozi 11 ambao jumla yao ni 111, hawa ndio watakaoenda kushindana ngazi ya mkoa na baadaye kupata timu ya mkoa itakayoenda kushindana kitaifa mkoani Mwanza.
Pia alisema pamoja na kufikia hatua hii ya mashindano, timu hizo zimekumbana na hali ngumu ya kifedha ili kupata timu hizo, alimuomba Mkurugenzi Mtendaji kwa kutumia mabaraza ya Waheshimiwa Madiwani waone ni namna gani wanaweza kusaidia kuwa na mfuko wa michezo wa wilaya kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya mapato ili miaka ijayo maandalizi yafanyike mapema na kwa ufasaha zaidi na hatimaye timu zetu zitafanya vizuri zaidi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa