• Wasiliana nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Baruapepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
Masasi District Council
Masasi District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
      • Asili ya Masasi
      • Historia ya Masasi Kiutawala
      • Orodha ya Viongozi
      • Ukubwa wa eneo
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za Kiuchumi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Maji
      • Ardhi na Maliasili
      • Usafi wa Mazingira
      • Maendeleo ya Jamii
    • Vitengo
      • Ugavi na Ununuzi
      • Sheria na Usalama
      • Nyuki
      • Tehama na Uhusiano
      • Uchaguzi
      • Ukaguzi wa ndani
  • Fursa za Uwekezaji
    • Agriculture
    • Construction Minerals
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Upimaji wa Ardhi
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
    • Huduma za kilimo
    • Huduma za mifugo
    • Huduma za uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Wah. Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha Utawala na Mipango
      • Uchumi Ujenzi na Mazingira
      • Kudhibiti UKIMWI
      • Maadili
      • Elimu Afya na Maji
    • Ratiba
      • Vikao vya Kisheria vya Halmashauri
      • Kuonana na Mhe. Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi Iliyokamika
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Sheria
    • Fomu za maombi
    • Jarida
    • Ripoti
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

LISHE KWA WATU WANAOISHI NA VIRUSI VYA UKIMWI

Posted on: July 4th, 2017


Binadamu wote wanahitaji chakula chenye kukidhi mahitaji ya kilishe ya miili yao.chakula huupatia mwili virutubishi mbalimbali kwa ajili ya afya bora ,ambayo ni pamoja na;

  • Kuboresha kinga ya mwilidhidi ya magonjwa mbalimbali
  • Kutengeneza  na kurudisha seli za mwili zilizokufa ,zilizochakaa au kuharibika
  • Ukuaji wa kiakili na kimwili
  • Kuupa mwili nguvu,joto na uwezo wa kufanya kazi

Ili mwili upate mambo yote hayo tunahitaji kupata mlo ulio kamili

Mlokamili:Ni mchanganyiko wa chakula kutoka kwenye makundi matano ya chakula ambayo huliwa pamoja na kwa kiasi kinachotosha. Makundi hayo ni;

  • Nafaka,mizizi na ndizi
  • Vyakula vya mikunde na vyenye asili ya nyama
  • Mbogamboga
  • Matunda
  • Mafuta na sukari
  • Maji si kundi la chakula ila ni sehemu muhimu ya mlo kwa ni huusaidia mfumo wa umeng’enywaji na ufyozwaji wa virutubishi kuwa rahisi.
  • LISHE KWA WENYE VVU WAKIWEMO WAJAWAZITO NA WATOTO
  • Lishe bora ni muhimu kwa watu wanaoishi na VVU kwani mahitaji yao ya kilishe yameongezeka kwa sababu ya maambukizi ya VVU huathiri ulaji, uyeyushaji, ufyonzwaji na utumikaji wa virutubishi mbalimbali mwilini, hivyo kupelekea matatizo yanayoambatana na lishe duni.
  • Hivyo Kwa watu wanaoishi na VVU wakiwemo wamama wajawazito na watoto inashauriwa wapewe angalau idadi ya milo 6 kwa siku yaani milo kamili mitatu na asusa mara 3.
  • LISHE  WAKATI MATATIZO MBALIMBALI YANAYOAMBATANA NA  VVU
  • Kukosahamu ya kula
  • Ongeza viungo kama tangawizi, limao, mdalasini, iliki n.k kwenye vyakula mbalimbali ili kuleta harufu nzuri kwa chakula na kuongeza hamu ya kula.
  • Kula milo midogomidogo mara nyingi kwa siku
  • Asitayarishe chakula mwenyewe au kukaa jikoni kwani harufu za vyakula hupunguza hamu ya kula
  • Kula vyakula na vinywaji unavyovipenda
  • Ikiwezekana asilepeke yake, ale pamoja na familia
  • Asinywe na kula kwa wakati mmoja kwani hii itasababisha tumbo kujaa haraka.
  • Afanye mazoezi mbalimbali ilikuongeza hamu ya kula.
  • Kichefuchefu au kutapika
  • Epuka vyakula vyenye viungo vingi, mafuta mengi au sukari nyingi.
  • Epuka pombe na vyakula vyenye kafeini kama  chai na kahawa.
  • Jaribu kula vyakula vikavu na vyenye chumvi kama mkate kwani upunguza kichefuchefu.
  • Kunywa maji,supu na vinywaji vya viungo kidogokidogo na endelea na vyakula laini.
  • Jaribu kula vyakula vilivyopoa.
  • Jaribu juisi ya limau. Au ndimu iliyochanganywa kwenye kikombe cha maji ya moto.
  • Kula wakati umekaa wima au jiegemeze kidogo kwenye mto. Usijilaze mara tu baada ya kula subiri dakika 30 hadi saa 1 baada ya kula
  • Usikae muda mrefu bila kula au kunywa chochote
  • Usile haraka kula taratibu
  • Muone daktari tatizo likizidi.

                                            

  • Kuharisha
  • Kunywa maji safi na salama kwa wingi. {Zaidi ya lita 2 kwa siku}
  • Kunywa vinywaji vya maji maji kwa wingi. Kama maji ya mchele, madafu, togwa,supu,juisi ya matunda na maji ya sukari na chumvi.
  • Kula matunda kama ndizi mbivu, tikiti maji na mbogamboga zilizopikwa, kama karoti, maboga na mchicha ili kurudisha madini na vitamin  zinazopotea .
  • Tafuna kwa muda mrefu au kula vyakula vilivyo laini kwa ni rahisi kumeza, kuyeyushwa na kufyonzwa mwilini.
  • Kula vyakula vyenye uvugu vugu nasio vya moto sana au baridi sana.
  • Epuka vyakula vyenye mafuta mengi, viungo vingi au pilipili nyingi. jihadhali kutumia matunda yasiyoiva vizuri, au yenye uchachu mkali, kwani wakati mwingine uongeza tatizo
  • Epuka vyakula na vinywaji vinavyosababisha gesi kwa wingi tumboni, kama maharage, kabichi na soda.
  • Epuka vinywaji vyenye kafeini, kama chai na kahawa kwani hivi usababisha upotevu wa maji Zaidi.
  • Epuka matumizi ya pombe kwani huzuia baadhi ya virutubishi kufyozwa nauonge za upotevu wa maji.
  • Epuka maziwa mabichi kwani yanaweza kusababisha kuharisha.
  • Ponda ponda vitunguu swaumu changanya kwenye kinywaji, kama supu.
  • Epuka vya kula vyenye Kamba lishe nyingi, kama nafaka na mikunde. Kwani haviyeyushwi kwa urahisi.hivyo kuongeza tatizo.
  • Mwone daktari tatizo likiendelea.

 

  • Kupunguauzito
  • Kuongeza aina ,kiasi cha chakula na idadi ya milo kwa siku
  • Kuongeza vyakula vyenye asili ya mafuta kama karanga, siagi na pia vyakula vyenye sukari kama asali n.k kwenye vyakula mbalimbali.
  • Kula vyakula vya nafaka kwa wingi kama mahindi, mchele, ngano, mtama, ulezi, uwele na viazi na pia aina za nyama, samaki na mikunde.
  • Kuweka viungo kwenye vyakula ili kuongeza hamu ya kula.
  • Kutumia vyakula vilivyochachushwa kama mtindi au togwa ili kusaidia uyeyushwaji na ufyonzwaji
  • Kufanya mazoezi mbalimbali ili kuongeza hamu ya kula.
  •  
  • Vidondakinywani au kooni na utandumweupekinywaji
  • Kula vyakula laini kama mtindi, uji au vyakula kama parachichi, papai,ndizi n.k
  • Epuka vyakula vyenye viungo vingi
  • Epuka vyakula vya moto au vyenye pilipili kali
  • Epuka vyakula vyenye sukari nyingi
  • Sukutua kinywa kwa kutumia maji yaliyochemshwa yenye vitunguu saumu au mdalasini. Rudia kilabaada ya saa 3 au 4.
  • Inapowezekana, tumia mrija wakti wa kula vyakula vilivyo katika hali ya kimiminika
  • Jaribu kumung’unya barafu, maziwa mgando/mtindi au embe mbichi kwani hivi hutuliza maumivu, kusaidia kupona na huzuia ukuaji wa utandu mweupe kinywani.
  • Kukosachoo au kupatachookigumu
  • Kunywa maji safi na salama mengi angalau lita 2 kwa siku
  • Tumia vyakula vinavyotokana na nafaka ambavyo havijakobolewa kama dona,nganon.k
  • Jaribu kufanya mazoezi kwani husaidia chakula kusagwa na kuyeyushwa kwa urahisi.
  • Kula matunda kama papai, parachichi au embe na mbogamboga kwa wingi kwani husidia kupata choo na kulainisha choo.
  • Mafua na kikohozi
  • Kunywa maji safi na salama ya kutosha
  • Tengeneza na kunywa vinywaji vingine vya limao, tangawizi ,kitunguu maji vilivyochanganywa na asali
  • Upungufu wa damu
  • Kula vyakula vyenye madini chuma kwa wingi kama vile samaki, nyama, maini, mbogamboga za kijani na vyakula jamii ya kunde kwa wingi.
  • Kula matunda kwa wingi wakati wa mlo hasa matunda yenye vitamin C kwa wingi kwani husaidia ufyonzwaji wa madini ya chuma mwilini. Kama mapera, machungwa, machenza, mapensheni, nanasi, mabungo, ubuyu, ukwaju, nyanya n.k
  • Epuka vyakula vyenye kafeini wakati wa mlo
  • Tibu magonjwa mengine kama malaria na minyoo
  • Matatizo ya Ngozi

Asilimia kubwa ya matatizo ya ngozi husababishwa na upungufu wa baadhi ya vitamin kama vitamin A na B6. Ingawa yanatibika kwa kutumia dawa, ulaji wa vyakula vyenye Vitamin A na B6 kwa wingi unaweza Kupunguza au kuzuia magonjwa hayo;

  • Mfano wa vyakula vyenye Vitamini A kwa wingini; Mboga zenye rangi ya kijani,  Mawese, Maini, Mayai, Maziwa, Papai, Karoti, Mabogan.k
  • Mfano wa vyakula vyenye vitamin B6 kwa wingini; Maharagwe, mboga zenye rangi ya kijani, karanga, mahindi, nyama,  parachichi n.k.
  •  

HITIMISHO

Ni muhimu kwa watu wanaoishi  na virusi vya UKIMWI kuzingatia ulaji wa chakula cha mchanganyiko na cha kutosha, pamoja na kuongeza idadi ya milo, kufanya mazoezi kutibu magonjwa nyemelezi mapema na kuzingatia usafi na usalama wa chakula na maji wakati wote.

  •  

 

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA MPIGA KURA MASASI DC 2025 January 14, 2025
  • MGAWANYO WA MAENEO YA UTAWALA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA TAREHE 27 NOVEMBA, 2024 MASASI DC September 18, 2024
  • MAENEO YA UTAWALA KATIKA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI September 18, 2024
  • FURSA YA MIKOPO INAYOTOLEWA NA MFUKO WA MIKOPO KUTOKA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO KWA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA MASASI November 12, 2021
  • Angalia Zaidi

Habari Mpya

  • MSIGWA: MAAFISA HABARI NI SAUTI YA SERIKALI, TANGAZENI MAFANIKIO YA SERIKALI KWENYE MAENEO YENU.

    May 25, 2025
  • MCHENGERWA: MAAFISA HABARI HAKIKISHENI MNAKUWA WABUNIFU NA WAZALENDO ILI WANANCHI WAPATE HABARI SAHIHI NA KWA WAKATI.

    May 23, 2025
  • MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MASASI DC KWA KISHINDO:WATEMBELEA MIRADI MITANO YENYE THAMANI YA TSH.MILIONI 678,844,040.00

    May 19, 2025
  • WATENDAJI WA SERIKALI TEKELEZENI WAJIBU WENU WA KIKAZI,MSIJIHUSISHE NA MAMBO YA SIASA: BARAZA LA MADIWANI

    May 15, 2025
  • Angalia Zaidi

Video

KAIMU MKURUGENZI MASUMBUKO MTESIGWA AKABIZI OFISI KWA MKURUGENZI MPYA
Video Nyingine

Kurasa za Karibu

  • RASIMU YA MPANGO WA BAJETI KWA MWAKA WA FWDHA 2021/2022 MASASI DC
  • Mpango Mkakati wa halmashauri ya wilaya ya masasi 2016/2017-2020/2021
  • Taarifa ya Hesabu ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha 2015/16
  • Rasimu ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 Masasi DC
  • Uchunguzi wa Madai ya Korosho kwa Misimu ya 2016/17 NA 2017/18 Wilaya ya Masasi
  • Mpango Kzazi wa Manunuzi kwa mwaka wa Fedha 2017-2018 Masasi DC
  • Mwongozo wa Malalamiko
  • Sheria

Kurasa Mashuhuri

  • Ikulu
  • Mtwara Region
  • Hati ya Malipo (Salary Slip)
  • Tamisemi
  • Sekretarieti ya Ajira
  • eGA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Masasi - Bomani

    Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi

    Simu ya mezani: 023-2510031

    Simu ya kiganjani: 023-2510031

    Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa