Kwa mujibu wa hotuba ya mgeni rasmi wa maonesho ya sikukuu ya wakulima nanenane 2017 waziri wan chi ofisi a rais TAMISEMI Mhe George Simba Chawene alisema kuwa Sekta ya kilimo ni sekta yenye mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi na wakulima kwa ujumla kama takwimu za mwaka 2015 zinavyoonesha kuwa sekta ya kilimo iliweza kuchangia pato la taifa kwa 29% na mwaka 2016 ikiwa ni 29.1%
Kwa upande wa chakula mwaka 2015 nchi ilikwa na utosherevu wa chakula kwa 123% na mwaka 2016 ilikuwa 120% nah ii imetokan na ongezeko la mazao ya chakula kwa 6.7% hivyo kilimo ni sekta muhimu sana katika kufikia uchumi wa kati kwani taifa lenye njaa haliwezi kujishughulisha katika shughuli za maendeleo.
Kwa upande wa ajira, sekta ya mifugo na uvuvi asilimia 65 watanzania wamejiajiri kupitia shughuli mbalimbali za kilimo mifugo na uvuvi. Hivyo kama sekta hii ikisimamiwa vizuri inauwezo wa kupunguza tatizo la ajira kwa watanzania wengi hususani vijana ambao ni nguvu kazi katika uzalishaji wa malighafi kwaajili ya viwanda vya ndani.
Pamoja na mafanikio makubwa ya kilimo wakulima wameendelea kuwa na changamoto kubwa ya kupata masoko ya uhakika ya kuuza mazao yao baada ya kuzalisha kwa tija. Uzoefu unaonesha kwamba mkulima anatumia nguvu na mali nyingi kuhakikisha anazalisha kwa tija lakini baada ya kuvuna hakuna soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao.
Kwa kipindi cha msimu wa mwaka 2016/2017 wakulima wamekuwa na changamoto ya kushuka kwa bei ya mazao mchanganyiko ikiwemo choroko, mbaazi na mengine yameuzwa kwa bei ya ndogo sana kutokana na bei ya soko kushuka bila kuzingatia gharama alizotumia mkulima katika uzalishaji, hali hiyo imewakatika tama wakulima wa maeneo mengi ikiemo wakulima wa masasi.
Katika kuhakikisha wakulima wanakuwa sehemu ya kutatua changamoto za ukosefu wa masoko hasa kwa wakulima, kampuni ya TEMNAR Company Limited inayojishughulisha na usindikaji wa mbegu za mafuta na kuzalisha mbegu imeamua kuwaelimisha wakulima kujikita katika kilimo cha Mkataba ili kujihakikishia soko la mazao yao.
Akizungumza wakati wa maaonesho sikukuu ya wakulima maarufu kama Nanenane mhasibu na mwelimishaji kutoka kampuni ya TEMNAR Company Limited bi Bahati Hassan Mohamed alisema kuwa kampuni yao iliamua kujikita katika kuelimisha wakulima kulima kilimo cha mkataba ambacho kinampa nafasi mkulima kupanga bei ya mazao yake na kampuni kabla ya kuzalisha hali inampa uhakika wa kuuza kwa faida tofauti na kutegemea soko huria ambalo halimpi mkulima nafasi ya kupanga bei japo amezalisha kwa tija.
Bahati alisema kuwa kampuni yao baada ya kuona wakulima wanapata shida ya masoko waliamua kuanzisha kilimo cha mkataba ambapo mkulima anazalisha akiwa anauhakika wa soko la mazao yake kwa kujaza mkatababa na kuuziana mazao kwa bei ambayo mkulima haimpi hasara lakini pia kuwawezesha kupata mbegu bora pamoja na kuwafuatilia kuhakikisha wanazaisha wa tija na viwango katika vikundi.
“Kilimo cha mkataba kimewavutia wakulima wengi alioweza kufikiwa na eimu hiii katika mikoa ya Mtwara na Lindi ambapo na wakulima wanazalisha kwa tija lakini pia wanapata faida tofauti na kuuza kwenye soko huria na kampuni inapata malighafi ya kutosha ya kusindika bidhaa za mafuta” alisema Bahati
Pamoja na kuwa mkulima anapata uhakika wa soko lakini pia kampuni hiyo inakuwa na uhakika wa kupata malighafi ya kusindika mafuta kutokana na mazao ya ufuta, karanga na alizeti. Hivyo kilimo hiki kinamfaidisha mkulima na kinafaidisha kampuni kwani mkulima anauhakika wa kuuza mazo yake lakini pia kampuni inauwezo wa kuzalisha kwa wingi kutokana na uwepo wa malighafi za uhakika.
Wakati tunawahamasisha wakulima kuzalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ni vizuri pia tukawahamasisha wakulima kujikita katika kilimo cha mkataba ambacho kitawahakikishia soko kwa mazao yao na hatimaye mkulima atajikomboa kupitia kilimo tofauti na hali ilivyo sasa ambapo mkulima hana nafasi ya kuuza kwa tija kama alivyozlisha kwa tija.
Ili kuitekeleza kwa vitendo kaulimbiu ya maonesho ya nanenane mwaka huu 2017 inayosema “Zalisha kwa tija mazao na bidhaa za kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa Kati” uzalishaji huu uende sambamba na uhakika wa soko kwa kujita katika kilimo cha mkataba ambacho kinamhakikishia mkulima kuona matunda ya alichofanya.
Hivyo makampuni ambayo yanahitaji kununua mazao kwa mkulima ni vyema yakaingia mikataba na wakulima walioko kwenye vikundi ili baada ya kuzalisha mfanyabiashara aweze kununua mazao kwa mkulima kwa bei waliokubaliana na sio kuwapangia kwani mauzo hayataenda kinyume na mkataba waliowekeana awali
Ili kufikia uchumi wa kati, mkulima aangaliwe zaidi asipangiwe bei na wafanyabiashara/mnunuzi , watumie begu bora, kuzuia ununuzi holela na kusimamiwa vizuri kulima kilimo cha kisasa ili mazao yanayozalishwa yawe na ushindani katika soko.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa