Kutokana na umuhimu wa lishe katika kujenga afya ya mwili, elimu inayohusu masuala ya lishe inapaswa kutolewa kwa kiasi kukubwa kwa jamii ili kujenga uelewa juu ya umuhimu wa kula Chakula bora au mlo kamili unajumuisha makundi matano ya vyakula ambayo ni nafaka, mizizi na ndizi, kundi la pili: vyakula vyenye jamii ya kunde na vyenye asili ya wanyama, kundi la tatu: mbogamboga, kundi la nne ni matunda na kundi la tano ni mafuta na sukari.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kamati ya lishe ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Bi Changwa M. Mkwazu wakati wa kikao cha kujadili taarifa ya utekelezaji kwa robo ya tatu na ya nne, na kubainisha kuwa watu wengi wanakumbwa na matatatizo ya kiafya yanayosababishwa na ukosefu wa lishe bora ikiwemo kwashakoo, marasmasi (unyafuzi) , upungufu wa damu wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano (Iron Deficiency Anaemia), Utapiamlo, kisukari, kukosa Vitamini na madini
Mkwazu alisema kuwa, kukosekana kwa elimu ya lishe bora kwa jamii ndio chanzo kikubwa cha watu wengi kushindwa kuelewa namna ya kuhakikisha wanakula chakula ambacho kina makundi yote ya chakula hali inayopelekea uwepo wa magonjwa na matatizo mbalimbali ya kiafya kwa jamii.
“Kwa Masasi vyakula ni vingi sana ila jamii haielewi kula kwa kufuata lishe bora badala yake wanakula ilimradi washibe tu, hivyo mtaalamu wa lishe ni lazima awaelimishe wananchi hususani akina mama namna ya kuandaa chakula chenye makundi yote matano kwa kutumia mazao waliyonayo na hatimaye tuwe na jamii yenye afya” alisema Mkwazu
Kwa elimu hiyo itasaidia jamii kuondokana na mazoea ya kula chakula cha aina moja badala yake watakuwa wanachanga au kubadilisha aina ya vyakula ili kuipa miili yao afya njema na pia kuepukana na maradhi mbalimbali yanayosababishwa na kuto kula chakula kinachozingatia mlo kamili/lishe,
Wananwake wajawazito wasipopata chakula kinachozingatia lishe bora wanahatari ya kupata magonjwa na uungufu wa damu hali ambayo imepelekea kiwango cha watoto wanaozaliwa na uzito mdogo chini ya kilo 2.5 kuongezeka sana na hivyo kuhatarisha maisha ya watoto hao.
Kwa uande wake meneja wake meneja wa mradi wa afya na lishe kanda ya kusini unaofadhiliwa na Agh Khan ndugu Anna Godfrey alisema kuwa kutokana na hali duni ya lishe ,kupitia shirika hilo wananwake wa vijijini wamekuwa wakielekezwa namna ya kuandaa chakula kinachozingatia lishe kwa kutumia mazao yaliyopo kama njia ya kujenga uelewa lakini pia kujenga utamaduni wa kula chakula ambacho kinazingatia makundi matano ya vyakula.
Meneja alisema kuwa pamoja na kufundishwa namna ya kuandaa chakula cha familia lakini pia wanafundishwa namana ya kuandaa chakula cha matoto kuanzia miezi sita na kuendelea ili waweze kukua vizuri na hivyo kuondoa maradhi kwa watoto kama utaiamulo na unyafuzi.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa