Kufuatia Mkoa wa Mtwara kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka 2018, Halmashauri ya Wilaya ya Masasi imechukua hatua ya kujipanga mapema kuhakikisha inakuwa na matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka 2019 kwa kupanga mikakati ya kuboresha ufundishaji ambapo walimu wa masomo mbalimbali watapigwa msasa.
Hayo yamebainishwa na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri hiyo ndugu Juma Kasandiko wakati wa kikao na wakuu wa shule zenye wanafunzi wa kidato cha tano na sita kilicholenga kuweka mikakati itakayopelekea wanafunzi wa shule hizo kufanya vizuri katika mitihani ya Taifa kwa mwaka 2019 na kuiletea sifa Halmashauri lakini pia na Mkoa kwa ujumla.
“Pamoja na kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha sita kwa mwaka huu 2018, bado tumeona tusiridhike na matokeo hayo, hivyo tumepanga kuwa na utaratibu wa walimu wa masomo ambayo ni magumu ikiwemo hesabu na kiingereza kupigwa msasa na walimu wenye uwezo mzuri kwenye baadhi ya mada ambazo ni ngumu ili kuwawezesha kufundisha vizuri” alifafanua Kasandiko.
Kasandiko alieleza kuwa kwa mwaka 2018, Halmashauri ya Wilaya ya masasi ilikuwa na shule moja tu ya kitado cha tano na sita ilyoshiriki mitihani ya kitado cha sita lakini kwa mwaka 2019 shule 4 zitafanya mitiani hiyo, hivyo ni vizuri kujipanga mapema ili kuhakikisha ufaulu unaongezeka zaidi.
“Naipongeza shule ya Ndanda Sekondari kwa kufaurisha wanafunzi wote 470 kwa daraja la kwanza mpaka la tatu na zuri zaidi hakuna daraja la nne wala sifuri ni kazi kubwa iliyofanywa na walimu kuwafundisha wanafunzi, nina imani kwa mikakati hii shule za Abbey, Ndwika na Chidya zitafanya vizuri pia” alieleza kasasndiko
Kati ya wananfunzi 470 walifanya mtihani na kufaulu, wanafunzi 395 walikuwa michepuo ya sayansi na 75 ni wa masomo ya sanaa hivyo inaonyesha kiasi gani walimu walitekeleza wajibu wao kwa kiasi kikubwa.
Aidha Kasandiko alibainisha kuwa kati ya wanafunzi 172 waliopata daraja la kwanza Kimkoa, wananfunzi 64 wametoka shule ya sekondari ndanda, kwa daraja la pili kati ya wanafunzi 848 wanafunzi 293 ni wa shule ya ndanda na kati ya wanafunzi 468 waliopata daraja la tatu 113 wametoka shule ya ndanda.
Akiongea kwa niaba ya wakuu wa walimu wengine mkuu wa shule ya sekondari Ndanda ndugu Mongate alisema kuwa kwa mkakati huo ana imani kuwa utaleta matokeo chanya kwa kuongeza ufaulu kwani kama walimu watakuwa na uwezo wa kufundisha mada zote kwa umahili mkubwa hali itakayowasaidia wananfunzi kufanya vizuri mitihani yao.
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa