MKURUGENZI MASASI DC AWATAKA WATUMISHI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi Ndg.Alphaxard Mashauri Etanga amewataka Watumishi kufanya kazi zao kwa kufuata taratibu na miongozo ya Serikali inayowataka kufuata kanuni za Utumishi wa Umma, na kutumia busara katika kuwahudumia Wananchi ambao ndio wateja wao.
Wito huo umetolewa leo tarehe 04/09/2025 na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo wakati akiongea na watumishi hao katika kikao cha kawaida kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo uliopo Mbuyuni Masasi.
Amesema Watumishi wanapaswa kujua haki na wajibu wao kwa kufuata Sheria, kanuni na taratibu za kazi pindi wanapotimiza majukumu yao na kuwa na nidhamu ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwahi kazini na kutoka kwa muda uliopangwa.
"Leo tumekutana hapa katika kikao cha kawaida kwasababu sisi kama watumishi mara kwa mara huwa tunakutana kwa ajili ya kuzungumza, kupata mawazo yenu na mwisho kwetu sisi viongozi tunatoa mwelekeo wa kiutendaji na tunahaidi kushughulikia changamoto na kero za Watumishi zinapojitokeza hivyo nataka mjue haki na wajibu wenu "
Aidha ameendelea kuwasisitiza watumishi hao
kushirikiana na kupendana katika kufanya kazi ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi wa Halmashauri hiyo.
Naye Mkuu wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali watu wa Halmashauri hiyo Ndg.Optatus Lusolela pamoja na kumshukuru Mkurugenzi kwa kutenga muda wake mara kwa mara kukutana na kuzungumza na watumishi hao na hatmaye kutatua changamoto zao pindi zinapojitokeza amewaomba watumishi hao kuzitumia fursa mbalimbali zinapotolewa na Halmashauri ili kujikwamua kiuchumi.
04/09/2025
Masasi - Bomani
Anuani ya Posta: S.L.P 60 Masasi
Simu ya mezani: 023-2510031
Simu ya kiganjani: 023-2510031
Baruapepe za Watumishi: ded@masasidc.go.tz
Hakimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Masasi. Haki Zote Zimehifadhiwa